25 June, 2014

WAZIRI PROF. MUHONGO ABANWA BUNGENI AELEZE KWA NINI UMEME UMEKATIKA NCHI NZIMA JANA

Kufuatia umeme kukatika ndani ya bunge wakati wa kupiga kura za kupitisha bajeti kuu ya serikali 2014/2015, hali hiyo imelikwaza bunge na kulazimu spika Anna Makinda kumtaka waziri wa nishati na madini kueleza sababu za tatizo hilo. 
Akizungumzia suala hilo bungeni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo aliomba radhi na kudai kuwa umeme haukukatika bungeni pekee bali ulikatika nchi nzima.
 Prof Muhongo alisema  sababu ya kukatika umeme ni mitambo ya kufua umeme inayotumia maji, mafuta na gesi imechoka ghafla na kwa mpigo hali iliyosababisha umeme kukatika kwa zaidi ya nusu saa. 
Aidha waziri huyo ameiagiza Tanesco kuomba radhi watanzania kwa tatizo hilo na kutoa maelezo ya kitaalamu ya kwa nini umeme umekatika nchi nzima haraka iwezekanavyo. 
Kukatika huko kwa umeme kulipelekea kukwama kwa zoezi la kupiga kura bungeni ili kupitisha bajeti kuu ya serikali.
hata hivyo zoezi la kupiga kura lilikamilika baada ya umeme kurudi ambapo wabunge 300 walipiga kura, kati yao 234 walisema NDIYO bajeti ipite na 66 walisema HAPANA isipite, hivyo bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kupitishwa. 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...