WOMEN'S CORNER


JAMANI GOLI LA ASUBUHI MPE MUMEO NI MUHIMU
Mwanaume anapoamshwa asubuhi,
inamwondolea uchovu, hata akil inachangamka,
hapo anakuwa kamili tayari kwa ajili ya
ujenzi wa taifa. Shoga, mpaka sasa hujaelewa
Mume anaamshwaje?

Unajua sana, hebu
nitolee umbeya huko!
Hii inawahusu sana wale wanawake ambao
wanatabia ya kuamkia kwenye majungu ya
vitumbua, maandazi ukiuliza eti ni biashara.utajiju Bibi Mwanaume anahitaji malezi sio ujanja ujanja

Hivi mwanaume akitoka nje ya ndoa kwenda kutafuta
kuamshwa utaweza kufanya biashara zako na zikaenda kweli?

Mwingine anadai anafanya usafi wa nyumba. Acha mambo hayo wewe. Jitulize hapohapo kitandani, mvutie baba watoto kwa mambo matamu, baada ya hapo hakikisha unampa kiamshio ili aamke.
Unaposhindwa kumuamsha mumeo asubuhi, unamwacha kwenye bahari yenye kina kirefu na unampa nafasi ya kuwa mzito katika kila jambo.
Kwa nini usimsaidie mwezako? Unataka huduma hiyo apewe na nani? Mwingine anaamka amechoka ati! Hebu acha mambo yako, kilichokuchosha nini..
Aliyekwambia
nani kama kiamshio cha asubuhi kinaongeza
uchovu?

MWANAUME ANAAMSHWAJE?
Ikifika alfajiri mwanamke kuwa wa kwanza kuamka kitandani, baada ya hapo fanya uchokozi wako kwa kumwamsha taratibu. Tena huo ndiyo muda wako wa kutumia utaalamu wako wote kuhakikisha anakuwa tayari kwa kupokea kiamshio kutoka kwako.
Endapo atapata kiamshio na umempa
inavyotakiwa, utakuwa umefanikiwa kumfanya
aamke akiwa amechangamka sawia na mawazo yake yote yatakuwa kwenye kazi.

Baada ya hapo, mpeleke bafuni akaoge, akitoka huko akute umeshamwandalia kifungua kinywa
kizuri. Hakikisha kina mvuto ambacho
anakipenda. Huo ni ushindi shoga.
Atakapotoka kwenda kazini, mawazo yake yote hujikita nyumbani. Aende nje kutafuta nini ikiwa
raha zote anakutana nazo nyumbani? Shoga
yangu, wengi wanasalitiwa kwa sababu ya kujisahau.

KWA WAVIVU
Kwa wale mnaoendekeza kazi za ofisini kama kigezo cha kuchoka, huo ni uvivu, itakula kwenu.
Eti unaamka alfajiri unawahi kazini je mumeo akitoka nje na kwenda kutafuta huduma mbalimbali utaweza kufanya hizo kazi kweli au ndiyo utalia na kusema umerogwa na vimada
usipendwe?

Wanawake wenzangu tuache visingizio kama
wewe unafanya kazi kumbuka mume ndiyo kitu cha kwanza kwani umewaacha hata wazazi
wako kwa ajili yake, kwa nini usimtimizie haki
zake kwa kufuata mienendo iliyo sahihi?

Kama una kazi za mbali au muhimu na yeye muweke kwenye ratiba ili usiharibikiwe upande mmoja.
Mume hapatikani popote bibi, si rahisi kihivyo Kazi zinatafutwa hata kwa kuhonga na utapata, lakini ndoa utamuhonga nani?
Je, utafanya nini
ili kumpata yuleyule uliyefunga naye ndoa?
Badilikeni mashosti ili kujenga nyumba ikae
salama.

Mwisho nikukumbushe kuwa karibu na mumeo
usiku wote. Mnapokaa sebuleni, talii kiwiliwili
chake kama mpiga gitaa, hapo utamsababishia
kukitamani kitanda, hivyo kulala mapema.
Mkiwa kitandani mapema, itawarahisishia
kufanya shughuli zenu mapema ili asubuhi
mkiamka, muendelee na kazi za ujenzi wa taifa.

  


Katika hali ya kawaida msichana au mwanamke hatazamiwi kuwa na ndevu kwenye kidevu, juu ya mdomo, kifuani, tumboni na mgongoni.


Kwa kawaida mwanamke huwa na vinyweleo vilaini, ambavyo jamii imezoea kuviita ‘malaika’.


Wanaume kwa kawaida huwa na ndevu ambazo huzitofautisha na vinyweleo kwa rangi nyeusi iliyokolea na huwa vigumu tofauti na vya wanawake ambavyo huwa vilaini.


Mwanamke anapokuwa na nywele nyingi sehemu hizo humaanisha kuwapo kwa hitilafu za kijenetiki au dosari za ulinganifu wa vichocheo vya jinsi mwilini mwake.


Wasichana wengine kutokana na urithi wa vinasaba, wanaweza kuwa na nywele nyingi sehemu mbalimbali za mwili. Hali hii kitabibu hujulikana kwa jina la ‘hypertrichosis’.


Mitazamo ya kijamii


Wanawake wanapoota ndevu nyingi hukabiliwa na changamoto za kisaikolojia kutokana na kuwa na mwonekano kama wa wanaume.


Mitazamo na mila nyingi za kijamii katika Bara la Afrika, bado zinakumbatia unyanyapaa wa wazi au wa kificho kwa wasichana wanaoota ndevu nyingi.


Msichana mwenye ndevu nyingi, anavuta hisia na macho ya wanaume na wanawake wenzake pia kiasi kwamba, anatazamwa kwa namna ambayo wakati mwingine inamnyima raha.


Wapo wanaume wanaoangalia wanawake wa namna hiyo kwa mtazamo hasi na wengine chanya. Ziko imani potofu miongoni mwa jamii kuwa wanawake wa namna hiyo wanaashiria kuwa na fedha, wengine wakiamini huwa wanawapiga waume zao na hata wengine kuamini kuwa hawana hisia za kike.


Ukweli ni kwamba wanawake wengi wenye ndevu huweza kuwa na hisia za kike kama wengine na hata kupata watoto licha ya mwonekano wa nje.


Wakati mwingine wanaume hawapendi kuoa wasichana au wanawake wenye ndevu nyingi kutokana na mwonekano unaowafanya wasichana hao kuwa kama wanaume.


Sababu za ndevu


Moja ya sababu za wanawake wengi kuota ndevu ni dosari za ulinganifu katika mfumo wa vichocheo vya mwili hasa vile vinavyoamua kutokea kwa mabadiliko ya ukuzi wa kijinsia.


Dosari za ulinganifu wa vichocheo vya kijinsia kwa wasichana zinaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuzalishwa kwa wingi kwa vichocheo vya ujinsia kutoka katika mifuko ya mayai na uvimbe katika mifuko ya mayai.


Uvimbe wa tezi ya Adrenali iliyo juu ya figo pia unaweza kusababisha tatizo hili kutokana na kuzalisha kwa wingi kichocheo cha Dehydroepiandrosterone (DHEA).


Wakati mwingine kunakuwepo na hali ya ulinganifu wa vichocheo vya ujinsia mwilini kama kawaida, lakini tatizo likawa ni mwitikio wa hali ya juu wa nywele kwa kiasi kidogo na cha kawaida cha kichocheo cha kiume kilichoko mwilini mwa msichana.


Katika hali hii, msichana pia anaweza kuwa na nywele nyingi sehemu mbalimbali za mwili wake.


Katika utafiti uliowahusisha wanawake 102 wanaokabiliwa na tatizo la kushindwa kutunga mimba waliohudhuria katika kliniki ya magonjwa ya wanawake, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kati ya Septemba 2006 na Februari 2007, ilibainika miongoni mwao, asilimia 32, walikuwa na uvimbe katika mifuko ya mayai.


Asilimia 56.3 ya wanawake wote wenye uvimbe huo, walikuwa na tatizo la kuwa na nywele nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kuota ndevu.


Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa Dk Pembe AB na Abeid MS wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Muhimbili (Muhas), uliochapishwa katika Jarida la Kisayansi la Tanzania, Journal of Health Research la Oktoba 2009.


Utafiti ulibaini kuwa mambo mengine yanayochangia kutokea kwa tatizo hili ni matumizi ya dawa za hospitalini na vipodozi vyenye viambata vya dawa kama testosterone na steroid.


Ikaonekana kuwa hayo ni matokeo ya matumizi ya muda mrefu ya kutumia vipodozi hivyo kwa muda mrefu bila kupata ushauri wa afya.


Matumizi makubwa na holela ya baadhi ya dawa zenye kemikali kama vile Danazol, Cyclosporin na nyingine pia yanahusika kusababisha tatizo hili.


Shirika la Habari la China (Xinhua), limewahi kuripoti taarifa ya mwanadada mwenye umri wa miaka 16 aliyejulikana kwa jina moja la Nana kuwa aliota ndevu nyingi baada ya kupewa matibabu ya hospitalini kwa kupandikizwa mafuta yanayopatikana ndani ya mfupa (uloto).


Mwanadada huyo alipewa matibabu hayo baada ya kupata tatizo la kupungukiwa damu mara kwa mara lijulikanalo kama Aplasticanaemia.


Wataalamu wa sayansi ya afya ya jamii pia wanauhusisha unene wa kupindukia kwa wasichana na kutokea kwa tatizo la kuota ndevu.


Unene wa kupindukia unaweza kusababisha ongezeko kubwa la kichocheo cha kiume kijulikanacho kwa jina la Androgen ndani ya mwili.


Hali hiyo hutokana na nyama zenye mafuta mengi kugeuza kichocheo cha kike cha estrogen kuwa kichocheo cha kiume cha androgen.


Androgen inapokuwa nyingi mwilini husababisha msichana kuwa na tabia za kiume ikiwa ni pamoja na kuota ndevu na kuwa na sauti nzito.


Daktari Adam Nyalandu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amewahi kunukuliwa kwenye gazeti moja la hapa nchini akisema kuwa tatizo la wanawake kuota ndevu linaweza kutokana na sababu nyingi ikiwamo matumizi ya vyakula vya kusindika vinavyotengenezwa kwa kutumia kemikali nyingi.


“Mfano ulikuwa huli nyama za kopo au vyakula vya kusindika ambavyo kemikali inatumika kuvisindika sasa unakula, vinaweza kusababisha tatizo hilo kwa kiwango kikubwa,” anasema Dk Nyalandu.


Wanawake wenye ndevu mara nyingi hukabiliwa na dalili kadhaa zinazowafanya watafute msaada wa kitabibu mara kwa mara. Baadhi ya dalili hizo ni kama vile kuota chunusi nyingi, kutokupata hedhi kama kawaida. Wakati mwingine msichana hupata damu pungufu wakati wa hedhi au kutoiona kabisa. Wataalamu wanasema wakati mwingine wanawake wa namna hiyo hupata hedhi isiyo na mpangilio.


Wanawake wenye tatizo hili pia wanakabiliwa na uwezekano wa kupata magonjwa sugu ya muda mrefu.


“Kama utafanya mahesabu, utagundua kwamba angalau nusu ya wanawake wenye tatizo la kuwa na nywele nyingi mwilini, wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupata magonjwa ya kisukari na moyo,” anasema.


Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa vichocheo vinavyohusiana na mfumo wa uzazi mwilini na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya cha Georgia, Dk Ricardo Azziz akielezea umuhimu wa utafiti alioufanya kwa kushirikiana na Vituo vya Afya vya Heather Cook na Kathleen Brennan, anasema matatizo mengine yanayosababisha ndevu kuota kwa wingi pia yanaweza kumfanya mwanamke kuwa mgumba.


Hali hiyo pia huweza kuandamana na kusinyaa kwa matiti na mfuko wa mji wa mimba. Athari nyingine ni pamoja na kututumuka isivyo kawaida kwa maumbile ya via vya uzazi na kuwa na sauti nzito na wakati mwingine kisanduku cha sauti hunenepa kama cha wanaume.


Mtawanyiko wa nywele mwilini huwa kama wa kiume. Pamoja na ndevu msichana huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi kwa wingi.


Epuka atahari kisaikolojia


Ili kuepuka athari za kisaikolojia zinazoweza kutokana na hali hii, msichana anashauriwa kuelewa kuwa kuota ndevu siyo dhambi na wala kosa.


Anapaswa kufahamu kwamba ndevu hazipaswi kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwani hali hiyo inaweza kuathiri afya ya mwili na akili.


Pia, ndevu zisiachwe zikawa ndefu kama za wanaume kwani zinavuta hisia za watu kumwangalia mwanamke au msichana kiasi kwamba hali hiyo inaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia.


Ndevu zikatwe na kuwa fupi kadri inavyowezekana wakati wote. Mkasi au cream ya kuondoa nywele inaweza kutumika kwa lengo hili. Ile dhana ya wanawake wengi kwamba ndevu zikinyolewa zinaongezeka maradufu haina ukweli wowote wa kisayansi.


Ndevu zising’olewe kwa vidole. Hii inaweza kusababisha uambukizo wa bakteria katika ngozi kwa urahisi na kuleta matatizo makubwa ya kiafya.


Njia nyingine iliyo bora kwa wasichana kujiepusha na tatizo la kuota ndevu ni kuachana na matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya steroidi vinavyoleta weupe bandia wa ngozi.


Kufanya mazoezi ya mwili na kudhibiti unene wa mwili kwa njia ya lishe bora pia ni mkakati mwingine unaosaidia kupambana na tatizo hili.


Endapo nywele zimetapakaa kwa wingi miguuni na mikononi na kuleta mwonekano wa kiume, ni bora kuvaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri ili kuepuka msongo wa kisaikolojia ambao unaweza kutokea kutokana na mtazamo hasi wa kijamii.



se

Mpenzi wangu ambaye nimedumu naye kwa mwaka mmoja leo amenitamkia kuwa hawezi kuendelea kuwa na uhusiano na mimi, amesema ameshndwa kuvumilia kuwa na mpenz bila kufanya S3X.

Amesema hawezi kunifanya pambo awe ananiangalia tu, lakn wakat tunaanza uhusiano alinikubalia kuwa hatufanya S3X mpaka tukifunga ndoa lakini leo amenigeuka. Nimelia saaana toka asubuh mpk asahv lakn naona haina maana, NAOMBEN ushaur wenu jaman nimrudie nikubal kuS3X nae au? 

Manake mpaka leo tayari nimeshaachika kwa wanaume kama wanne yote chanzo ni S3X, sasa nitaachika mpaka lini? Manake inavyoonyesha ni kwamba wanaume hawawezi kukaa na mwanamke bila ku-s3x kama atakwambia yupo tayari kukaa na wewe hivyohivyo huwa wanakuwa na wanawake wengine wa nje wanao s3x nao.

Nilishaurini jamani, nimwambie nipo tayari ku-s3x nae au niachane nae tu? Ukweli nampenda sana .




SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA

Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga

VISABABISHI
i. Bacteria
Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.
ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)

iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.

iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.

v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.

vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhulu.

JINSI YA KUJIKINGA
• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.
• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.
• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.
• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.
• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.

CHANZO UJANA NA MAHUSIANO COMMUNITY

Miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto mchanga chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:

  1. Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
  2. Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
  3. Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti na kizazi.
  4. Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu na ghalama.
  5. Maziwa ya mama ni raisi kupita kwenye mfumo wa chakula wa mtoto na umsaidia kuwa na akili nzuri
  6. Husaidia katika uzazi wa mpango   

KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE: Kuwa mwanamke ambaye anahitajiwa na mwanaume na sio mwanamke anayehitaji mwanaume.

KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE(1) Kuwa mwanamke ambaye anahitajiwa
na mwanaume na sio mwanamke anayehitaji mwanaume.Tafsiri
yake Kibaologia ubongo wa mwanaume una tofauti kubwa ukilinganisha na
wa mwanamke na hivyo utendaji wao na mahitaji yao yana utofauti pia.
Uwezo wa kuzungumza wa mwanamke ni mkubwa kuliko wa mwanaume,yaani kwa
siku moja mwanamke ana uwezo wa kuongea maneno 20,000
wakati mwanaumeana uwezo wa kuongea maneno 7,000 kwa siku. Mwanamke
asipojua njia za kuoanisha tofauti hizi atamchukiza mwanaume bila ya
yeye kujua na ndio maana Biblia inasema "kila mwanamke mwenye hekima
huijenga nyumba yake. Bali aliyempumbavu huibomoa kwamikono yake
mwenyewe (Mithali 14:1).Ili uweze kuwa mwanamke ambaye mwanaume
anamhitaji inakupasa usome mahitaji ya mwanaume vizuri ili uweze
kuyatimiza kikamilifu na kumtosheleza kabisa.(2) Mwanaume
akikuacha au kukudharau ni hasara yake na sio yako.Tafsiri yakeIwapo
una uhakika wa kuifuata vizuri kanuni ya kwanza na kwabahati mbaya
ukapata mwanaume asieuona uthamani wako usibabaike kabisa. Yeye ndie
kipofu haoni thamani yako na kuandoka kwake toka katika maisha yako
maana yake Mungu anakuelekeza kwa mwanaume mwingine aliye bora kuliko
huyo. Biblia inakuagiza "Tulia ujue ya kuwa mimi ni Mungu nitatukuzwa
katika mataifa" Zaburi 46:10.(3) Onekana kama kipepeo lakini
ng'ata kama nyuki.Tafsiri yakeBiblia inasema kwamba wanawake wanapaswa
wajipambe kwa utu wa moyoni usioonekana yaani roho ya upole na utulivu
na hekima (Petro 3:4).Mwanamke pamoja na mapambo yote na uzuri wa nje
ni muhimu tabia yake ionyesheutulivu na upole. Kipepeo haumizi mtu na
anapendeza kwa muonekano wake lakini hivyo peke yake haitoshi kuvuta
na kutunza penzi la mwanaume. Hivyo basi ni muhimu mwanamke mara
nyingine awe kama nyuki, yaani aonyeshe ukali pale anapoonelewa.
Ajenge uwezo wa kuelezea hisia zake bila ya uoga wowote ule.KUMBUKA
kuwa wanaume hupenda wanawake wanaoleta changamoto zinazojenga na sio
wenye unafiki.Kwa kufanya hivyo ataweza kudumisha penzi katika
msingiwa haki na ukweli na sio unafiki. Fuata maneno ya BWANA YESU
"kuweni na busara kama nyoka na wapole kama njiwa (Mt 10:16).(4)
Usianzishe ugomvi bali zifahamu njia za kumaliza ugomviTafsiriUkiwa
mpole utapenda sana kutafuta kumwelewa mwenzio badala ya
kumhukumu,ukimhukumu hasira huja haraka na hivyo kuanzisha ugomvi.
Epuka kukurupuka na kusema maneno harakaharaka.Jifunze kutulia japo
umeumia au kukasirika. Kwa kufanya hivyo utaweza kuona kwa urahisi
njia za kujibu na kutatua migogoro katika mahusiano yako. (5)
Kuwa mpenzi na sio mpiganaji lakini siku zote pigania
unachokipendaTafsiriUnapoamua kuwa na uhusianowa kimapenzi na mtu
jitahidi kumpa mapenzi yote kwa moyowote. Pamoja na hayo yote
yatokeapo magumu kuwa mstaarabu kuepuka hali ya ugomvi kwa kujizuia
kupaza sauti au kuongea maneno makali. Jambo la msingi tambua mambo
muhimu na usikubali mpenzi wako ayapuuzie mambo hayo kwa urahisi.
Jenga hoja nzito za kupigania haki yako ya kuishi maisha ya furaha na
amani.(6) Kupata kitu ambacho hujawahi kukipata ni lazima ufanye
vitu ambavyo hujawahi kufanya.TafsiriNi rahisi sana kufanya vitu
ulivyozoea na kufurahia hali hiyo mpaka pale itakapotokea shida fulani
inayohusiana na kitu ulichokizoea .Ili uweze kuendelea kufurahia
uhusiano wako zaidi ni muhimu utafute vitu vipya vyakupamba na
kuimarisha uhusiano wako. Hapa inahitaji ubunifu, uchunguzi na ujasiri
wa kujaribu jambo ambalo hujawahi kukutana nalo. Kwa kuwa kila siku
tunakutana na mambo mengi upo uwezekano mkubwa wa mtu kubadili mtazamo
wake juu yako na ukapata matatizo katika uhusiano wako. Kuleta vitu
vipya huleta msisimko mkubwa na iwapo wewe ndio utakuwa chanzo cha
msisimkohuo basi utathaminiwa na kupendwa zaidi.(7) Kabla
hujauliza kwanini fulani hakupendi, jiulize kwanini unajali sana juu
ya hilo. TafsiriKumpenda mtu mwingine ni kitu rahisi sana na sisi wote
tumo katika kundi hilo lakini kumfanya mtu mwingine akupende au
aendelee kukupenda sio rahisi kabisa.Pale unapotamani mtu fulani
akupende kwanza jiangalie mwenyewe vizuri je kama mtu huyo anapenda
mtu mwenye maumbile mazuri unayo sifa hiyo?. Kama anapenda mtu mfupi
wewe unayo sifa hiyo? Na kama anataka mtu mwenye elimu au mwenye pesa
wewe umo kwenye kundi hilo.? Hayo yanaweza kuwa maswali magumu kwa
wengi lakini swali lingine rahisi kwa kila mtu ni je ni kwa vipi mimi
nitaweza kuchangia furaha yake zaidi ya mtu mwingine yoyote?. Ukiweza
kujibu swali hili unanafasi kubwa ya kujisogeza kwake na yeye akakuona
kuwa kweli unafaa, lakini ukijisogeza bila kuwa na sifa za kutosha
unatafuta maumivu ya moyo. Madhaifu kama aibu, hasira, woga,
unenekupita kiasi, uvivu au kupenda kuongea bila ya kuchoka yanaweza
kuharibu penzi hata kama utapata mtu mwenye penzi la kweli. Jichunguze
kama vile Biblia isemavyo." Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na
angalia asianguke (1Wakorintho 10:12)"Jijaribuni wenyewe kwamba
mmekuwa katika imani, jithibitisheni wenyewe (2 Wakorintho 13:5).

ZIFAHAMU DAWA ZA NYWELE NA VIPODOZI VINAVYOSABABISHA UVIMBE KWENYE KIZAZI CHA WANAWAKE


Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zikipendwa na wanawake wengi wa Afrika, hasa wa Tanzania kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kuzifanya zipendeze na kuvutia sana.


Mvuto wa nywele zilizotiwa dawa
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zina madhara makubwa sana kwa afya ya mtumiaji. Kwa mfano, wanadai kuwa zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali zinazotumika kuzitengeneza dawa hizo. Kemikali hizo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka dawa hizo na hivyo kusababisha madhara makubwa kwenye kizazi.
 
Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe uitwao “fibroids” au “leimyoma” kwenye kizazi.
“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu na husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.
 
Dk Chipata anasisitiza kuwa huwa uvimbe kwenye kizazi hutokea  na kukua sana katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi, yaani kabla hajakoma hedhi.

mwanamke akitengenezwa nywele huku wengine lukuki wakingojea kwa hamu muda wao  wakutengenezwa ufike

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.
 
“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvimbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.
 
Dk Chipata anasema madhara yanayotokana na kemikali za vipodozi ni makubwa sana, siyo tu kwenye kizazi bali huweza hata kusababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).
 
“ Kemikali za dawa za nywele si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua, bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi ya mtumiaji” anasema.


  vidonda vilivyo sababishwa na dawa za nywele kuunguza ngozi ya kichwa wakati wa kupaka
Dk. Chipata anashauri kuwa ni vyema  na salama zaidi watu kubaki na ngozi pamoja na nywele halisia, yaani ambazo hazijapakwa dawa au vipodozi hivyo. Hili likishindikana, basi watu wasome maandishi yaliopo kwenye kopo ama boksi la vipodozi na dawa za nywele ili kubaini vimetengenezwa kwa vitu gani kabla ya kuvitumia.  
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.
 
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.



Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.
 
Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.
 
Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?

Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.
 
Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.
 
Uvimbe kwenye kizazi ni nini?
Ukuta wa nyumba ya uzazi umejengwa kwa misuli ya tishu. Kwa kawaida uvimbe huu huanza kidogo kidogo na hukua hadi kufikia ukubwa wa tikiti maji. Fibroids kubwa huweza kukua na kutanua nyumba ya uzazi na kuwa sawa na ujauzito wa miezi sita au saba.
 
Mwanamke huweza kuwa na uvimbe mmoja mkubwa au vivimbe vingi ndani ya kizazi.
 
Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa Kitengo cha Upasuaji cha Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili, Henry Mwakyoma anauelezea fibroids ni uvimbe ambao upo katika umbile la misuli myembamba na laini linalokua siku hadi siku.
 
“Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake,” anasema.
 
Dk Mwakyoma anafafanua kuwa, vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.
 
“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika umri mkubwa au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni,” anabainisha mtaalamu huyo.

“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa wake. Wengi hugundulika wakati wa kujifungua au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi,” anasema.
 
Anaongeza: “Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,”
 
Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.
 
Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.
 
“Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakaona dalili zote za mimba na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,” anasema.
 
Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara kuzuia uuzwaji wake.
 
Isitoshe akasema: “Elimu inatolewa kwa wananchi pia ili kuwafahamisha kuhusu madhara ya vipodozi hivyo kwa sababu wanunuzi wasipokuwepo basi hata biashara haitakuwepo.”
 
Pamoja na hayo, adhabu hutolewa ya kuwanyang’anya na kuwapeleka mahakamani wenye maduka makubwa wakiziuza.

JINSI YA KUSAFISHA UKE WAKO... WADADA HII INAWAHUSU SANA!
Awali nilikuwa nikidhani kuwa kila mwanamke anapaswa na anafahamu jinsi ya kujisafisha ndani ya uke mara tu baada ya kuondolewa bikira (kuanza mahusiano ya kimapenzi na hatimae ngono), lakini nimekuja kugundua ukweli kwamba wanawake wengi hawajui uke unasafishwa vipi?

Baadhi huofia kuwashwa na sabuni na wengine hudhani utokwaji wa utoko ni kawaida hivyo hawana budi kuacha kama ilivyo na badala yake hutumia “pads” ndogo au “wipes” zenye manukato ili kuzuia harufu/shombo ya uke na vilevile kuzuia uchafukwaji wa “vyupi”.

Huitaji kuficha (Bali punguza) harufu ya asilia ya uke kwa kutumia bidhaa zenye mahukato hasa ukiwa na mpenzi wako kwani hiyo harufu ndio uanamke wenyewe na ikikutana na ile ya kiume ndio raha ya kufanya mapenzi na ikiwa mpenzi wako ni “aliyejaaliwa” atakuwa akiipenda harufu hiyo na hubaki akilini mwake hali inayoweza kumfanya akupende zaidi au kutoweza kufanya ngono na mtu mwingine bali wewe.

Hujawahi kusikia wanaume wanashindwa kutoka (date) wanawake wengine baada ya wapenzi wao kufariki dunia? Au mwanaume kushindwa kuendelea na maisha yake ya kimapenzi bila wewe na matokeo yake hata mkiachana lazima atarudi tu kwako….sababu moja wapo ni hiyo.

Kujiswafi ili kupunguza ukali wa shombo/harufu ya uanamke:
Utoko hujikusanya ikiwa mwili umetulia (usiku) hivyo hakikisha unajisafisha kila asubuhi kabla hujaanza kuoga.
Kwa wale tunaoishi Bongo wengi tunatumia maji ambayo usalama wake ni wa utata, sasa ili kuepuka maambukizo hakikisha maji ya kujisafishia sehemu zako za siri yamechemshwa vizuri. Unaweza kutenganisha maji ya kuoga na ya kusafishia uke ukitaka.

*Kabla huja anza kusafisha  uke wako hakikisha umesafisha mikono yako vizuri kwa sabuni (ukiweza tumia sabuni yenye dawa) na wakati huo huo pitisha sabuni juu ya uke wako ili kuondoa vijidudu kama vilikuwepo, safisha mahali hapo(juu ya uke kwa maji na hakikisha hakuna sabuni).

*Kisha kwa kutumia kidole chako cha kati, ingiza taratibu pale ambapo uume unaingia, kwa kuanzia huitaji kwenda mbali sana. Zunguusa kidole hicho taratibu huku ukijimwagia maji kwa kutumia mkono wa pili, kisha kitoe (kitatoka na weupe mzito) safisha kidole na maji yako.

*Rudia tena na sasa kiingize ndani zaidi na ukizunguushe tena (huku ukijimwagia maji) na kukitoa utaona “utoko” mwingi zaidi kidoleni, rudia hatua hizo mpaka uhakikishe kidole kinatoka bila weupe(utoko) na utahisi hali ya usafi, hakuna utelezi.

Unapojimwagia maji ukeni huku kidole kiko ndani maji huingia pia ukeni na ndio maana mwishoni kabisa utahisi umesafishika vema kabisa na utoko huo hautotoka tena siku nzima na uke wako hautokuwa na shombo kali kama ambavyo siku zote ambazo ulikuwa hujisafishi.

Kwa wale wanaotumia “bath” au “shower” unafanya kama nilivyoeleza ila tofauti ni kuwa maji yataingia vizuri zaidi ikiwa unapata “bath” hivyo hakikisha “bath” sio ya kuchangia, maji ni salama(safi), usiweke sabuni (bath cream) au bidhaa yoyote yenye kemikali kwenye “bath” yako ili kuepuka matatizo ya kiafya na maambukizo mengine.

Ikiwa unaswali, nyongeza, ushauri, maoni kuhusu mada hii na nyingine zilizopita na hasa zinazomhusu mwanamke tafadhali niandikie kupitia:  jojothefighter@gmail.com.
 

KAULI NANE AMBAZO MWANAMKE AKIZITOA JIHADHARI SANA


1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.


3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.

4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.


5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.


6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.


7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.


8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza

JE, NI KWELI KUWA KILA MWANAMKE ANAJIUZA NA SIO WALE TU WANAOSIMAMA BUGURUNI?? 

Huu ni ukweli hata tukipinga hakuna mwanamke asiyejiuza tofauti kuna aina mbili tu za hii biashara.

1. Wale wanaojiuza kwa kutafuta wateja kusimama mabarabarani.
2. Hawasimami barabarani wanaenda kwa special order, kufahamiana kwanza kama urafiki, kupitia mitandao, kukutana kwenye bar na magari n.k

Ukitaka kujua kuwa wote hawa wanajiuza, mlale mwanamke halafu usimpe noti uone zali litakavyokuwa! Fanya uchunguzi hapahapa jijini Dar, nakuhakikishia ni wanawake wachache sana labda 2%-10% ambao hawako kibiashara juu ya mapenzi.

1. Kuna demu mzuri sana anafanyakazi (ofisi kubwa) ya sirikali mshahara wake ni zaidi ya Tshs m2 kwa mwezi anabwana ake tena wameshibana lakini juzi tu akawa anataniwa na rafiki yangu mmoja mwenye nchi ndafuu sana kuwa nataka kukuoa, kama vipi uje home tuonje tunda bana, tena demu aliweka mafuta yake akaja na gari yake akavurugwa kisa uanjua nini hapa?? Pesa huyu anajiuza ila yeye ni kwa investiment huyu ni MUWEKEZAJI!!

2. Kuna demu anasoma chuo kikuu anatamba sana kwenye mitandao na kuweka picha ya bwana ake kila mara juzi kati mchizi wangu kamuanzishia chat kwa fb mpaka muda huu kashatoa uroda biashara ni ileile kila akitaka kutoa nauli, alipewa mara ya kwanza elfu 20 alikasirika sana, huyu ni mjasiriamali.

3. Nenda Bar yoyote Dar, hata mhudumu unayemuona anajiheshimu akikuletea soda au bia yako mnong'oneze mwambie nina lfu 50 tukalale wote, hakikisha una simu maana tayari mzigo umepata hii nayo ni biashara anauza sema tu ni parti time.

4. Usimuone mmama wa makamo mkubwa na mkurugenzi wa kampuni fulani mwambie ninajua kula mzigo lazima utampata tu wewe usiogope sura yake na heshima yake ongea tu, huyu naye anauza sema yeye ni doner.

5. Mademu karibia 80% Dar wanamabwana zaidi ya 5 kila mmoja amepengwa kisawasawa, kweli anao watano aende buguruni kufanya nini? 


Source: Mkereketwa


BAADA YA MZEE MAJUTO KUMTEMA MKE WAKE,MKE HUYO KAENDA KUSHITAKI BAKWATA

SIKU chache baada ya
ndoa ya supastaa wa
vichekesho Bongo, Amir
Athuman ‘Mzee Majuto’
kuvunjika, mke
aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam
Tanzania (Bakwata)
kutoa malalamiko yake,
 
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee
Majuto, Septemba 14,
2013 alikimbilia Makao
Makuu ya Bakwata
Wilaya ya Kinondoni
yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana
huyo, mambo
aliyoyazungumza
kwenye ofisi hiyo ni
matatu, kwanza kutopewa talaka baada
ya kuachika.
Akasema akimuuliza
Mzee Majuto kuhusu
talaka yake anamwambia
amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema
amfikishie, akahoji:
“Kwani huyo Rehema
ndiye aliyenioa?”
Pili, akasema wakati
anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo
alimwachisha kazi mahali
na pia alimhamisha
kwenye chumba
alichopanga. Tatu, akasema kutokana
na hayo yote anaomba
alipwe fidia ya fedha kwa
sababu ya usumbufu
alioupata.
Rehema akasema kutokana na malalamiko
yake,
viongozi wa
Bakwata walimpa barua
ya kumfikishia Mzee
Majuto yenye kichwa cha
habari cha WITO.
Mzee Majuto anatakiwa
kufika bila kukosa
kwenye ofisi hizo,
Septemba 23, mwaka
huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na
mwanamke huyo
lizungumzwe. Kwenye
utetezi wake, mzee huyo
alisema alimwacha
mwanamke huyo baada
ya kugundua hajatulia.

 KAULI YA LADY JAYDEE BAADA YA KUNUSURIKA KUANGUKA JUKWAANI
"Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali zingine, isitoshe sikuanguka bali nilikaribia. Ila poleni kwa mlioumizwa na hicho kitendo... Nitapunguza urefu wa viatu siku nyingine"

USIOLEWE KWASABABU HIZI...

Usiolewe Sababu Rafiki Zako Wote Wameolewa.
Usiolewe Sababu Class Mates Zako Wote Wameolewa Na Wanawatoto.
Usiolewe Sababu Umemaliza Chuo, Unaishi Mwenyewe Na Unakazi Nzuri.
Usiolewe Sababu Kila Mtu Kanisani Anakuuliza Pilau Tutakula Lini.
Usiolewe Sababu Wazazi Wanataka Kumuona Mkwe Na Wajukuu.
Usiolewe Sababu Wazazi Na Wewe Mmechoka Kuchanga Sasa Mnataka Kuchangiwa.
Usiolewe Ili Uonekane Umeolewa.
Usiolewe Kwa Sababu Umepata Ujauzito.
Usiolewe Sababu Unaogopa Kuzeeka Ukiwa Mwenyewe.
Usiolewe Sababu Unaona Umri Unakwenda.
Ndoa Sio Jumuia, Ndoa Sio Destination, Ndoa Sio Zawadi Kwa Wazazi, Ndoa Sio Social Status, Ndoa Sio Watoto, Ndoa Sio Kuondoa Nuksi..
Olewa Kwa Sababu Ni Wakati Wa Mungu Wewe Kuolewa, Umempata Mtu Sahihi Mnayependana Kwa Dhati, Umeridhia Kutoka Moyoni Bila Kuwa Influenced Na Kitu Chochote..
Ni Bora Uendelee Kuishi Mwenyewe Kuliko Kuingia Kwenye Ndoa Ya Majuto. Mngojee Bwana Na Hakika Hatakuacha Wala Hajakusahau.

SIFA 10 ALIZONAZO MWANAMKE AMBAZO MWANAUME HANA
  • Ana uwezo wa ku 'pritend' katika mahusiano kwa muda mrefu
  • Hata kama hana biashara au hafanyi kazi yoyote, ana uwezo wa kupendeza
  • Akipenda, anapenda kweli
  • Ana nguo nyingi zaidi kuliko mwanaume
  • Akiwa na mtoko, kucha na nywele ndio kipaumbele cha kwanza
  • Ni mvumilivu sana ila maji yanapofika shingoni chochote kinaweza kutokea na kuwa katili sana
  • Ana oga mara nyingi zaidi kuliko mwanaume
  • Ni mwepesi kusamehe na kurudisha moyo nyuma hata kama ametendwa kiasi gani
  • Akiwa na familia, watoto wake huwa ndio jicho lake (hana jadi ya kutelekeza watoto)
  •  Ni mwepesi kutoa siri zake za ndani kwa marafiki na hicho ndicho kinawa 'cost' baadae

IMARISHA MAPENZI YAKO, KWANINI UWE MTU WA KUACHWAACHWA KILA SIKU??

# Jaribu hv halafu uone itakuwaje.

1. Ukishampata mpenzi baada ya kutongozana kwa muda mrefu usiridhike endelea na unyenyekevu uleule.

2. Ukimtazama machoni hebu jaribu kukumbuka ulivyoktana naye na kipi kilikufanya umpende. Usijizoeze kusahau chanzo cha mapenzi yenu.

3. Hebu jizoeze kumfikiria alivyoumbika. Usimfananishe na mwingine atakosa ladha upesi.

4. Akikukosea hebu kumbuka mema aliyokutendea. Msamehe!

5. Kila siku uwe mpya kwake, aidha chumbani ama hadharani. Kuwa mbunifu.

6. Cheza cheza naye, hakuna kitu kizuri kama utoto, basi fanyaneni watoto. Mtafurah nyie! Mfano michezo ya kujificha au hata kupigana kiutani utani.

7. Muheshmu mpenzi wako. Halafu ficha siri zake basi.

8. Penda kuandamana naye, itamfanya ajiskie wa muhimu kwako. Akiwa mbali usijidai umeizoea hali.    Lalamika tena sana tu!

9. Kwa lolote hata dogo mwombe ushauri. Mh! Atavimba kichwa huyo na atajenga imani kwako.

10. Kama mna ahadi ya kukutana naye, subiri kila kitu ufanye ukiwa naye mfano kula, kuoga na hata kulala. Usimwache mpweke!
 


KWA WADADA WANAOJIANDAA KUOLEWA.
#Vidokezo jinsi ya kuish na mawifi na mashemeji.

Pand hz mbili ndo huwa kikwazo na chanzo cha 'ndoa' nyingi kuvunjika, sasa ili kudumisha ndoa zao fanya mambo haya.
WIFI. Huyu akikutembelea nyumbn kwako, mpokee vizuri, jichekeshechekeshe, ucmpe makazi magumu magumu ya kufanya, akiwa na kashda kidogo we mpe vipesa, vile viatu vyako vizuri kama vimekubana we mpe na hata kale kagauni mpe, halafu akivaa mwambie 'AMEPENDEZA', Akikuambia ishu za ki-mbea mbea we muunge mkono. Usimwamshe mapema asubuh mwache aamke anavyotaka. Siku akiwa anaondoka mpe kitenge ampelekee mama mkwe kijijini, nauli atakuwanayo lakini mpe kisirisiri pesa ya ziada. Atakupenda huyo, atakufaglia kwa kaka yake hadi raha.

SHEMEJI. Hawa dawa yao ndogo, akiwa amekuja kumsalimia kaka yake ama mdogo wake, wewe hakikisha mambo ya chakula yanakwenda kwa wakati, tena chakula kiwe cha kutosha anakula hadi kinabaki. Mashemeji wanapenda kula asikwambie mtu, hawa huwa hawana maneno meng hawataki pesa yako, wewe pika chakula akija anakikuta mezani. Yaani atakusimulia huko atakapokwenda 'ah! Mke wa bro ndo mke bwana!!' akiulizwa sababu hasemi, kumbe ni msosi!! Hapa unakuwa umem2liza.

MAMA MKWE. Huyu ukiweza kuwabana mawifi na mashemeji huwa hana kelele, kwa hyo usihofie. Hatakusumbua!

#Via....Shoga havai sketi hata kama anapenda kuwa mwanamke!

Ukizingatia haya utakua mrembo daima
  • Pata muda wa kutosha kupumzika
  • Fanya mazoezi
  • Kula mlo kamili
  • Kunywa maji yakutosha
  • Tumia vipodozi sahihi kwa ngozi yako
  • Badilika kutokana na mazingira

Lingo to Inspire Women 
  • The way you dress will determine the way you will be addressed
  •  Dress to look good and not cheap
  •  Your nails are your details, keep them neat
  • Self confidence is talking less and listening more
  • Live in such a way that you will be celebrated and not tolerated
  • Real beauty begins in your mind
  • A lady of prayer is a lady of power
  • Live to learn not just to earn. Work harder on yourself than  on your job
  • Meekness is never a weakness, but strength expressed in a wiser manner

Tabia zinazochangia  wanaume kukukimbia
1. Umalaya
2. Uchafu
3. Uongo
4. Kutojali

Mwanamke Hulka
  • Jifunze kutunza siri
  • Unachozungumza ndicho kitakachokutambulisha
  • Sikiliza pande zote kabla hujazungumza
 

Tabia zinazofanya watu wakae mbali na wewe
Majivuno: Kujisikia na kujiona wewe ndio  bora kuliko wengine kutakusababishia ukose marafiki na watu wa kua nao karibu.
Kuzungumza sana: Kila kitu kinapozidi huwa kinaharibu. Chumvi tunaitumia kuleta ladha kwenye chakula, lakini chumvi hiyo hiyo inapozidi hufanya chakula kisifae kuliwa. Kuzungumza sana kunapelekea kuongea mambo ambayo hayakupaswa kuzungumzwa mbele ya watu wanaokusikiliza.
Ushindani: Katika mavazi, urembo ni mambo yanayowagharimu wasichana wengi. Kwasababu Fulani amevaa  hiki au kile basi na wewe unataka. Ushindani huu ungetumiwa katika masomo au mendeleo ya uchumi  ingesaidia kwani ushindani m baya huzaa wivu na chuki miongoni mwa watu.
Uvivu: Hupelekea kushindwa kuwajibika na kutimiza majukumu uliyopaswa kufanya.  Mwanamke mvivu hupelekea hata mazingira yake ya nyumbani, mwili wake au watoto wake kutoyajali. Hii ni hatari sana kwa familia na jamii kwa ujumla
Uongo:  Ni dhambi ya tatu (3) katika mtiririko wa amri 10 za Mungu;  Kwa kesema uongo haimaanishi umemaliza tatizo bali umeairisha kwani siku ukweli utakapokuja kujulikana, hali itakua mbaya zaidi na utasababisha kuto aminiwa tena.
Ugomvi: Kuna wanawake bila kugombana hawaoni raha, jambo dogo watalikuza liwe kubwa ili mradi tu kutokee ugomvi. Tabia hii itakufanya watu wakae mbali na wewe. Hata majirani watakutenga na marafiki watakukimbia.
Umbea: Kuzungumza mambo ya watu wengine  yasiyokuhusu, huo ni umbea.  Wanawake wengi wakikaa lazima wamzungumzie fulani… Le kava  vile, kapika hichi, hiyo ni tabia mbaya. Fahamu ya kwamba huyo uliye kaa nae kumsema mwingine, ipo siku atakaa na wengine kukusema wewe.
Dharau:  Dunia ni duara, aliyekupa wewe gari la kutembelea, nyumba nzuri ya kifahari, fedha za matanuzi  isikufanye ukamdharau anaetembea kwa miguu, anayeishi kwenye nyumba ya kupanga, asiye na fedha za kumfanya apate hata mlo mmoja. Binadamu wote ni sawa.

Jivunie kuumbwa mwanamke
Katika maisha yangu yote, sijawahi kujutia kuzaliwa mwanamke. Namshukuru Mungu kwasababu kuwa mwanamke ni jambo jema. Na kama mwanamke nimegundua uzuri wa ndani na nje  niliojaliwa na muumba.
Nashangaa kuona wanawake wanaojutia kuumbwa wanawake! Kwa hakika hao bado hawatambui wanachosema.
Tumezoea kuona vipaumbele vingi wanapewa wanaume. Kwa mfano tukizungumzia Afrika, asilimia kubwa ya wanawake bado hawajapewa nafasi ili waoneshe uwezo wao walionao katika maswala mbalimbali ya maendeleo katika jamii kiwemo siasa, uchumi, teknolojia, michezo, burudani  n.k lakini tumesahau kwamba mwanaume aliyepewa nafasi na kuonekana ndie bora;  ametoka kwenye tumbo la mwanamke.
Kinachotugharimu sisi wanawake ni kimoja tu, HATUPENDANI. Yaani ukimuona mwanamke mwenzako kafanikiwa  huwa ni tatizo.
Jiamini unaweza kufanya chochote. Kuna usemi siku hizi umevuma “mwanamke akiwezeshwa anaweza” mimi nina amini hata asipowezeshwa anaweza. Mwanamke ni kiungo muhimu katika familia na jamii kwa ujumla hivyo kamwe usijishushe.

Sifa 15 zinazomfanya  mwanamke avutie
  • Ukarimu
  • Heshima
  • Uaminifu
  • Kujituma
  • Ujasiri
  • Unyenyekevu
  • Upendo
  • Uvumilivu
  • Uwazi
  • Nguvu ya ushawishi
  • Moyo wa Kusamehe
  • Upole
  • Usafi
  • Kujifunza

Unachokivaa, ndicho kitakachokutambulisha.
Katika ulimwengu huu , naamini wanawake ndio waliojaaliwa kuwa na mitindo mingi zaidi ya mavazi na urembo  kuliko kwa wanaume. Kwa maana ya kwamba mavazi ya wanawake ni pamoja na magauni, sketi, suruali (jeans & kitambaa), t shirt, blauzi, wakati kwa wenzetu wanaume wao ni suruali (jeans & kitambaa) peke yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba mavazi yote anayovaa mwanaume yanaweza kuvaliwa na mwanamke; wakati mwanaume hawezi kuvaa mavazi anayovaa mwanamke. (labda shoga)
Inatakiwa utambue mavazi gani unatakiwa uvae wapi. Usichanganye mavazi ya nyakati / sehemu nyingine ukayavaa  nyakati/ sehemu nyingie.
Fahamu mavazi ya ofisini, mavazi ya michezo, mavazi ya ufukweni, mavazi ya kwenye sherehe mbalimbali, mavazi ya kwenye burudani n.k
Inashangaza kukutana na mwanamke akiwa amevaa mavazi ya usiku nyakati za mchana! Hata kama utapendeza lakini  utachekwa na watu huko barabarani.

Maeneo  muhimu  zaidi  ya mwanamke kuwa safi
  • Kucha
  • Nywele
  • Ngozi
  • Mwili kwa ujumla

Nini kinatokea unapopingana na jinsi ulivyo?
Kama hujipendi wewe mwenyewe hakuna atakaevutiwa na wewe wala kukupenda. Kwanza jikubali, jipende na kamwe usitamani kuwa kama mwingine. Tamani kuwa wewe. Usijilinganishe na mwingine…
Jambo la msingi ni lazima ufahamu uzuri wa mwanamke huanzia ndani. Kwa maana ya kwamba  anavyokula, tabia yake, anavyojifunza na kutenda  ndivyo vinavyopelekea mwanamke kuonekana mzuri; Hata hivyo siamini kwamba kuna binadamu  m baya.
Kutojikubali kwa jinsi ulivyoumbwa ni sawa na kumkosoa Mungu aliye kuumba.  Soko la madawa na vipodozi limeongezeka  kwa kiasi kikubwa kutokana na idadi kubwa ya wanawake  kutumia bidhaa hizo ili kubadilisha muonekano wa sura, maumbo yao. Ni makosa makubwa hasa kwasababu madhara yake ni makubwa kuliko faida.
Mwanamke anapoamua kujichubua, kuongeza makalio au matiti  hajajikubali jinsi alivyo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...