Albert
Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni
kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Kwa
mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa
vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa
darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo.
Hawana akili, japo wana elimu.
Einstein
alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini
hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili
ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.
Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.
Akili
siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni
elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani
na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti.
Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza
kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?
So
mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye
elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia
akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.
Yeye
ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona
"kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao.
Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa
wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.
Usijidharau
kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye
degree 4.
Kumbuka
Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote
uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki
na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako
kinabaki na nini?
Kama
kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI".
No comments:
Post a Comment