23 September, 2014

MR. BLUE: NIPO TAYARI KUFANYA COLLABO NA DIAMOND AU ALIKIBA?

Hivi sasa katika mitandao ya kijamii wasanii wanaobattle kwenye vichwa vya habari na kutengeneza ‘kick ya story’ ni Diamond na Ali Kiba.
Kwa hiyo ni kawaida mstari mmoja unaowahuwahusu kutengeneza story ya aya tano kwa kuwa wanapendwa sana na mashabiki.
Rapper wa Micharazo na BOB amekutana na swali hilo wakati anaongea na mtandao mmoja wa kijamii ambao ulitaka kupata mtazamo wake ni yupi kati ya wakali hao angependa kushirikiana nae kwenye wimbo wake hivi karibuni.
“Unajua mimi wale wote washikaji zangu na wala sina tatizo nao, kwa hiyo niko tayari kufanya kazi na yeyote yule ambaye atakuwa tayari. Si unajua hii kazi na kazi mkishirikiana pamoja ndio inakuwa nzuri zaidi.” Amesema.
Mr Blue anaetarajia kuachia video muda  wowote zilizoongozwa na Adam Juma, Pesa na Mapenzi.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...