Prof.
Ibrahim Lipumba, aliyekua mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) alitangaza
kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Akizungumza
jijini Dar es salaam, Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano
yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema
Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba
iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta
hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya
Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Prof.
Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa
kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.
No comments:
Post a Comment