14 January, 2014

WEMA AMREKODI DIAMOND KITANDANI

SINI ya malovee inaendelea! Penzi lenye historia ya kushamiri, kumwagana na kurudiana limezidi kuchukua sura mpya, safari hii, Wema Sepetu ‘Madam’ amenaswa akimrekodi video ‘bebi’ wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Sosi ya kuvuja kwa sini hiyo mpya ilitokea Ijumaa iliyopita ambapo bila hiyana, bibie Wema aliamua kuitupia video katika Mtandao wa Instagram ambayo alimrekodi Diamond aliyekuwa akiandika mashairi kitandani, akamsumbua kwa kumrekodi huko na kusindikiza kwa ujumbe uliosomeka:
“In da middle of his writing session…just had to disturb him a little”(Katikati ya muda wake wa kurekodi...nikamsumbua kidogo).
Diamond aliyekuwa akiandika mashairi, alisumbuliwa na Wema kwa kumrekodi huku akimtaka aweke mapozi tofautitofauti hali iliyomfanya ‘boyfriend’ wake huyo waliyerudiana siku chache zilizopita, apoteze umakini wa kuendelea kuandika mashairi.
Baada ya muda mfupi, ‘posti’ hiyo ya Wema ilipata maoni kibao huku kila mmoja akiweka mtazamo wake. Kuna ambao walimpongeza kwa kufurahi kuona uhusiano wao huku wengine wakiponda kuwa wamechoka ‘drama’ zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...