15 January, 2015

SALA ILIYOKUTWA KWENYE KABURI LA YESU MWAKA 1503 AD



Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami.

Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu, Utuhurumie
Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu, uwe kinga yangu
Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu,  uniondolee maumivu yote makali.
Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu, uniondolee dhambi zangu zote.
Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu, nitembee nawe katika njia ya wokovu.
Ee Msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu, unikinge kutoka hatari ya kifo cha milele.
Naahidi kujitahidi daima kuabudu msalaba Mtakatifu wa Yesu Kristu.
Ee Yesu wa Nazareti uliyesulubiwa msalabani unihurumie. Nakuomba unikinge wakati wote na pepo wabaya wasiniguse.

Ee Mama wa msaada wa daima nayaweka maombi yangu mbele yako nikiwa na dhamira nyeupe kama mtoto ninaomba msaada wako.
Ee Mama Mpendelevu, nakuomba ujionyeshe kwangu sasa, unionee huruma.
Ee Mama Mpendelevu, Mama wa Msaada ninakuomba kwa ajili ya upendo wako Mkuu uliompenda Mwanao Yesu Kristu, na kwa ajili ya heshima ya madonda yake Matakatifu, ninakuomba unisaidie katika lazima zangu .................................... (taja mahitaji yako)
Ee Mama Mpendelevu nakukabidhi mahitaji yangu yote katika jina la Mungu Baba.
Ee Mama Mpendelevu nakukabidhi mahitaji yangu yote katika jina la Mungu Mwana.
Ee Mama Mpendelevu nakukabidhi mahitaji yangu yote katika jina la Mungu Roho Mtakatifu.
Mama yetu wa Msaada daima utuombee x 3 Amina.

MAELEZO:
Baba Mtakatifu alimtumia Mfalme Karoli Sala hii wakati alipoenda kupigana vita na maadui wa Ufaransa.
Inaaminika kuwa mtu yeyote anayesali, au anayemsikiliza mwenzake akisali au anaechukua sala hii mfukoni mwake ataokolewa kutoka kifo cha ghafla, kuzama majini, Kuunguzwa na moto, kulishwa sumu, kushinda vita au kushikwa mateka.
Akiwa Mwanamke mwenye mimba anasali sala hii, au akishiriki kwa unyenyekevu katika kusali sala hii, au akiwa na nakala ya sala hii, Bwana Yesu atamsaidia azae mtoto kwa urahisi. Mtoto anapozaliwa na mama yake akiweka nakala ya sala hii upande wa kulia wa mtoto wake, mtoto huyo atakingwa na mabaya yote. Ikiwa unatembea njiani na ukamwona mtu yeyote mwenye kifafa, iweke nakala ya sala hii upande wa kulia wa mgonjwa huyo na atapona mara moja. Bwana Yesu amesema “Mtu yeyote atakayejitahidi kuiandika sala hii na kusambaza kwa watu wengine nitambariki.” Na pia Bwana Yesu anaendelea kusema “Yeyote atakayepuuza sala hii ataangamia”. Kama nakala ya sala hii inahifadhiwa katika nyumba. Yesu atakinga nyumba hiyo na hatari ya Radi, Ngurumo, au kuporomoka kwa nyumba. Mtu yeyote anayesali sala hii kila siku, Yesu atamwashiria kifo chake siku tatu kabla.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...