03 May, 2014

JE UNAMJUA ALIE ACT SINEMA YA 'YESU? MSOME HAPA CHINI...


Sikukuu ya Pasaka imekwisha  ila najua watu wengi nikiwemo hata mimi mwenyewe huwa napenda kuangalia Sinema ya YESU, na sinema hii huwa maranyingi inapendwa na watu wa marika yoote bila kujali Dini zao na watu wengi wanampenda sanaa huyu mwigizaji wake mkuu kiasi kwamba watu wengi wanadhani ndio sura halisi ya Bwana YESU kutokana na jinsi alivyouvaa uhusika! Leo nimeona nikudodosee kidogo kuhusiana na mwigizaji huyu, Huyu jamaa ni Mmarekani aitwae JIM CAVIEZEL, alizaliwa Mount Vernon Washington Marekani mwezi Sep 26 1968. Mwigizaji huyu japokuwa amlizaliwa Marekani lakini asili yake ni baba Mswiss na mama kutoka Slovakia.

Yaap hii ndio picha ya Cover ya Sinema hiyo ya 'YESU' ambayo iliongozwa na Mwongozaji maarufu wa Movie nchini Marekani ambaye ninamzimia sanaa MEL GIBSON iitwayo The Passion Recut...

Yaani ukiiangalia Movie hii ya 'Passion of Christ' inahuzunisha na kufurahisha na mimi binafsi nayapenda sana maneno ya 'YESU' yenye Tungo na Methali nyingi kwa wabaya wake, Naipenda sanaa na huwa sichoki kuitazama mara kwa mara...

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...