Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
23 May, 2011
DINI NI BIASHARA
Bila shaka yeyote atakae fanikiwa kupitia waraka wote kwa makini atakubaliana na mimi kwa asilimia 100% kwamba dunia ya leo, Dini imekua biashara katika makanisa yaliyo mengi nchini na nje ya Tanzania.
Kabla sijashuka na mtiririko na data zote ili niudhihirishie uma juu ya tamko langu, nawaomba radhi wale wote watakao kerwa hasa kwasababu waumini wengi huwaambii kitu kuhusu dini, watumishi au makanisa yao!! Napenda pia kutoa angalizo kwamba si makanisa yote wala si watumishi wote wa Mungu wanafanya dini kama biashara. Bali hao wanaofanya wamewatia doa wale ambao hawahusiki na tuhuma hizi.
Idadi ya watu wanaokwenda kusoma ili waje kuwa Wachungaji, Mapadri imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Umeshawahi kujiuliza ni kwanini??
Rafiki yangu aliwahi kwenda katika kanisa moja maarufu hapa Dar es Salaam ili kuabudu Jumapili hiyo lakini alishangazwa na kitendo cha wasimamizi wa kanisa kumwambia asikae kiti cha mbele kwani pale ni V.I.P. kwa utafiti niliofanya niligundua kwamba wale wanaokaa zile siti za mbele ni waumini wanaotoa sadaka kubwa!!
Inawezekana waumini wengi hawafahamu uchakachuaji wa SADAKA zitolewazo na waumini makanisani. Sisemi uache kutoa sadaka!! Hembu tujiulize, pamoja na sadaka zoooote tunazotoa tena kwa makanisa mengi, kuna sadaka ya 1 sadaka ya 2 mpaka sadaka ya 3 katika ibada moja!! Yaani muumini mmoja anatoa sadaka mara 3. Hiyo ni kwa Juma pili tu!! Bado ibada za wiki!! Hii sio biashara?? Kuna wakoma, na walemavu tunaokua tukipishana nao barabarani wakiomba misaada kwa wapita njia. Mara ngapi tunawapita kama vile hatuwaoni?? Hivi sadaka zinazotolewa makanisani zimeshindwa kufanya chochote kwa watu hawa??
Ninavyofahamu mimi, makanisa mengi yamefadhiliwa hivyo hupokea misaada mingi, lakini pamoja na hayo, sadaka wanazotoa waumini makanisani husaidia shuhuli mbalimbali na mahitaji muhimu ya watumishi wa Mungu. Kuhimizwa kutoa sadaka imekua kama kibwagizo makanisani mwetu leo hii. Eti “ukitoa kidogo, utapata kidogo” Jamani jamani… Mh!
Imekua ni kaaida watu wengi kukimbilia katika makanisa yanayotangaza kufanya miujiza ili wapate utajiri, ajira, na wengine wapone magonjwa sugu kama vile UKIMWI, Kansa, Kisukari, Presha, Utasa, Ugumba na mengine mengi. Ukweli ni kwamba watu wengi wanakimbilia na kutafuta uponyaji wa roho huku wakisahau kabisa kwamba MWILI si kitu bali ROHO. Lakini kwasababu tunaishi ulimwenguni ni vema na busara mtu akawa na afya njema ili awe na nguvu na uwezo wa kufanya kazi ambayo itamsaidia katika mahitaji.
Sikatai watu kuponywa kwasababu hakuna mtu anaependa kuugua na ndio maana tiba ya Babu Loliondo imekua gumzo duniani kote. Hii yote ni kwasababu watu wanapenda kuwa na afya njema siku zote. Swali la kujiuliza: Je, tuna uhakika gani juu ya maombezi tunayoombewa ili kupata utajiri n.k? Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini wapo wengi wanaoombewa makanisani lakini hawaponi?? Na ndivyo hivyo hata wale wanaokwenda mahospitalini kupata matibabu sio wote wanaopona??
Hujawahi kujiuliza kwanini baadhi ya watu waliokwenda kupata tiba kwa babu Loliondo HAWAJAPONA? Jibu ni rahisi… Kila jambo na wakati wake: Si lazima kila mtu anaekwenda kupata matibabu au maombezi apone siku hiyo hiyo au aponyeshwe kwa kuombewa na Mchungajii Fulani. Biblia inasema mnaangamia kwa kukosa maarifa. Kisa cha Ezekia katika Biblia ukisoma 2 Wafalme 20 tunaelezwa jinsi Mungu alivyo KATAA kumponya Ezekia kwa kusudi maalum…Kwasababu aliona akirudisha uzima wake angemkufuru Mungu hivyo kuikosa Mbingu!!
Nikupe kisa kingine kilichotokea Uingereza ambapo kuna kijana mmoja alipata taarifa kwamba mama yake mzazi yu taabani; hivyo ikambidi kijana yule aende airport ili afanye utaratibu wa kusafiri, alipofika akaambiwa hakuna nafasi, alilalamika sana kwani alitaka awahi ili akapate angalau maneno ya mwisho ya mama yake. Kama haitoshi alirudi airport kesho yake ili aangalie kama kuna mtu angalau atakua ameahirisha safari ili apate nafasi asafiri, lakini haikua hivyo. Pale alimlaumu sana Mungu na kuona kama Mungu hamtendei haki. Haikupita muda vyombo vya habari vikatangaza kutokea kwa ajali ya ndege iliyoua watu wote waliokuwa ndani ya ndege ile ile ambayo kijana yule alikua anataka kusafiri nayo. Hapo akaona kumbe Mungu anampenda!!
Mimi ni Mkristu na ninaamini Mungu yupo na ninaamini ipo siku atarudi kulichukua kanisa yaani wale waliovumilia mpaka mwisho, tena walio tenda mema hapa duniani kwa kumpendeza Mungu na wanadamu pia. Mungu awabariki na kuwaongoza katika kutambua makanisa yaliyopo kwa ajili ya kufanya biashara tuyaepuke kwani yanatupeleka pabaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
Nurath Sakuru likes this
ReplyDeleteHassan Iddy: ulikua ujui aina vat wa ushuru
ReplyDeleteMecky Massawe: Hamuogopi wachungaji/paroko/padri/wainjilisti watafunga na kuomba kwa ajili yenu? au nyie hamna dini
ReplyDeleteTengia Vitalis: Hilo ni Jibu tafuta swali?
ReplyDelete