Hii sio hadithi wala tungo... Ni kweli yamenitokea.
Nipo katika computer tokea saa nne usiku wa jana! Na sijatoka mpaka sasa hivi saa kumi na moja alfajiri na sitarajii kutoka mpaka muda wa kwenda chuo ufike. Haijawahi kutokea nika kaa kwenye computer usiku kucha kama nilivyofanya leo japo huwa ninakaa kwenye computer muda mrefu lakini si usiku hasa usiku wa manane!!
Leo nitaiweka katika kumbukumbu zangu kwani kilichonitokea leo hakijawahi kunitokea tokea nizaliwe... Pengine nianze kudadavua kilichonisibu mpaka nikaamua kuandika ujumbe huu wa "sitaisahau siku ya leo 19 May 2011"
Mwanafunzi mwenzangu ambae ni mjasiriamali mwenzangu Dennis Mwasalanga aliniazima modem yake (modem yangu sikua nimei recharge)kwa miadi kwamba nitamrudishia kesho asubuhi... pengine hiki ndio chanzo kilichonifanya leo nikeshe!!
Ilipofika saa kumi alfajiri nilihisi nimekanyaga maji miguuni mwangu!! Si tukio la kawaida wala mazingira ya mimi kukanyaga maji sehemu niliyokua nimekaa nikifanya kazi zangu...!!
Nilipata mshtuko wa ajabu lakini hata hivyo nilijipa moyo wa ujasiri nikachukua biblia nikasoma Zaburi ya 45!! Halafu nikapata wazo la kuwapigia simu ndugu zangu ili niwape taarifa ya maajabu yaliyonitokea hasa kwasababu naishi peke yangu.
Wa kwanza kumpigia alikua ni mama yangu mzazi ambae simu yake ilikua imezimwa, nikatuma msg kumpa taarifa ili atakapoiwasha akute ujumbe wangu...
Mtu wa pili kumpigia alikua dada yangu ambae alinielekeza nikemee na kusoma Zaburi ya 46!! Nikashangaa kwani awali mimi nilifungua Zaburi ya 47 na nilikua bado sijafunga ukurasa ule, hivyo alivyoniambia nisome Zaburi ya 47, fasta nikasoma!!
Sikuishia hapo, nikaamua kumpigia baba simu ili amuamshe mama (wapo Moshi)ili mama afungue simu na asome msg niliyomtumia... kwamba nimejikuta nimekanyaga maji, hali ambayo si ya kawaida...
Mtu wa tatu kumpigia simu alikua dada Happy ambae ni mwanafunzi mwenzangu yeye ana kipawa cha maombezi, na ninamkubali sana!! Hapo ilikua inaelekea saa kumi na nusu usiku! Haikuchukua muda mrefu dada Happy alipokea simu yangu nikamueleza mkasa ulionipata... nae aliniongoza sala nikaisali, baada ya hapo akaniambia nikachukue maji katika kikombe nikafanya hivyo... akasali kisha akaniambia nimwage kiasi cha maji katika maji yale niliyokua nimeyakanyaga huku nikiita DAMU YA YESU na JINA LA YESU, kisha akanielekeza kiasi cha maji yaliyobakia niyanywe... nikafanya hivyo...
Wakati dada Happy anasali kupitia simu, mama yangu mzazi nae alikua anapiga simu mfululizo nami sikuweza kupokea kwasababu nilikua naogea na Happy, baadae nikapokea simu ya mama nae akaniongoza sala nikasali. Na sasa naendelea na kazi zangu isipokua nimevaa ndala kwasababu ya maji maji chini ya miguu yangu (hapa katika computer)ninayoendelea kufanyia kazi zangu... Duh leo! Ni siku ambayo sitaisahau maishani
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
Nicodemo Ngimba: nimesoma kilicho kutokea pole nguvu ya bwana itaishinda nguvu ya giza
ReplyDeleteMuddy Mosha: dah pole sana kwa mkasa huo jose,mungu bado yupo nawe coz umeonyesha imani kubwa kwake nae hawezi kukuacha
ReplyDelete