20 September, 2011

WANAPAITA GEREZANI... WANAPAITA MNADANI

Ilikua ni baada ya kujiuliza maswali mengi kuhusu usalama wa raia wa Tanzania na usalama wa mali za raia wa Tanzania una umuhimu gani kwa vyombo husika vilivyopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanaendelea kuishi kwa wasiwasi na mali zao hasa magari kwasababu ya wizi unaofanyika na baadae soko la mali zao zilizoibiwa kwenye magari yao hasa vioo (site mirror) na taa za magari yao kisha kuelekezwa mahali ambapo wanaweza kuvipata!

Wanapaita gerezani.... wanapaita mnadani huko ndipo vifaa vyote vya magari vilivyoibiwa vinapatikana huko. Tena ukifika wanakugombania kama njugu. Mamlaka husika imeshindwa kulisimamia hili? Kukomesha na kuwa wajibisha watu hawa  jamani!? NI KWELI IMESHINDIKANA??

Siamini! Au wananchi tuamue kujichukulia sheria mkononi? Na kutoa hukumu ya kifo kwa wale wanaotuumiza? Tutawezaje kusema MIAKA HAMSINI BAADA YA UHURU mamlaka husika zimeshindwa kudhibiti hata uhalifu wa wazi wazi namna hii!!










Tunazitaka mamlaka husika zisikie sauti hii; sauti ya wananchi waliochoshwa na kuibiwa mali zao na kwenda kuzipata gerezani. Ushahidi kutoka kwa wananchi waliowahi 'kulizwa' na watu hao wanaoiba vioo na taa za magari na kwenda kuviuza gerezani wanasema imekua kawaida.... yamekua mazoea, na hata wale wanaokamatwa kwa uhalifu huo huwa hawachukui muda wanatoka mahabusu  na kuendelea na uhalifu  mtaani pasipo kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Upo mpango madhubuti utakaochukuliwa endapo KILIO CHETU kitaendelea kufumbiwa macho.
Na kuzibiwa masikio. Hakika Tanzania bila vibaka yawezekana. Kama kubarikiwa Tanzania ilishabarikiwa!

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...