20 February, 2012

NIMEKUA SUNGUSUNGU WA GARI YANGU MWENYEWE

Natengeneza historia mpya ya maisha yangu baada ya kukesha kulilinda gari langu usiku kucha ili kunusuru mchezo mchafu uliotaka kuchezwa na mjanja mmoja wa mjini.
Mchezo ulianza hivi: Wiki iliyopita jirani yangu ambae alinizoea ghafla katika kipindi kifupi ambae aliamua kunifundisha udereva wa gari yangu (Manual) ambae pia alionyesha ujirani mwema kwa kuniambia niwe  nalaza gari langu kwao kwa usalama zaidi.

Nilikuja kugundua mchezo wake mchafu alipoanza kuniambia mara hiki, mara kile kimeharibika; Kumbe vifaa anavitoa kwenye gari yangu mwenyewe na kuniuzia mimi mwenyewe; Hakuishia hapo; Jana sasa! Asubuhi nilitoka na gari nikaenda kwenye mizunguko yangu nikarudi jioni, huku nikimsubiri jirani yangu huyo ili aje kuingiza gari ndani. Nikiwa ndani na mgeni wangu (mjumbe wa nyumba 10) majira ya saa 4 usiku tulisikia kishindo kama gari imefungwa! Sikushtuka kwasababu nilikua na fungua za gari yangu. KUMBE ALIKUA NA FUNGUO BANDIA

Punde baadae jirani yangu akagonga mlango kuniita tupeleke gari kuli park kwao. Akaniambia leo utaliingiza mwenyewe, kwa kawaida huwa analiingiza na kulitoa yeye kwasababu sehemu gari linapoingia ni pembamba sana, mpaka inabidi kufunga vioo vya sight  mirror ili gari iingie.

Sikum bishia, nikapanda kwenye gari, ile nawasha gari HALIWAKI! Nilipatwa na mshangao hasa kwasababu niliporudi nalo kutoka kwenye mizunguko yangu lilikua halina hitilafu yeyote. Kumbe jirani huyo alionekana akifungua gari na kuchomoa vifaa 3 vijulikanavyo kama Relay!

Akaanza kuangalia angalia pale na kuniambia nimpe hela ili akavilete! ( Hii  haikua mara ya kwanza kunifanyia mchezo huo) Nilipomshtukia kwamba ametengeneza mazingira ya gari yangu isiwake niliamua kumwambia aondoke, nikalinda gari mpaka asubuhi....!!

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...