16 February, 2012

Watendaji wachakachua mpango wa Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete amestushwa na kuvurugwa kwa mpango wa ujenzi wa nyumba za watendaji wa Kijiji cha Msoga mkoani Pwani, tofauti na makubali...ano na wanakijiji wa kijiji hicho miezi michache iliyopita.

Akizungumza jana katika kambi ya mafunzo ya vijana zaidi ya 400 iliyoasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, Rais Kikwete alisema ameshangazwa na mabadiliko hayo aliyoyaelezea kuwa ni kinyume na makubaliano ya wanakijiji wa Msoga.

“Nilipokuwa nakuja huku kwenye hii kambi, nilijua kwamba ujenzi wa nyumba za watendaji wa tarafa hii, ungekuwa upande ule (akionyesha upande wa pili wa barabara), lakini nashangaa misingi ya nyumba imeanza kuchimbwa huku, ni kinyume kabisa cha makubaliano yetu,”alisema Kikwete.

Alisema kuwa anashangazwa na mabadiliko hayo yaliyofanywa kinyume na mpango ambao yeye kama mwanakijiji wa kijiji hicho na wenzake walikubaliana ambapo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kulifanyia kazi suala hilo.

“Mama Mahiza ni nini kimetokea hapa, mbona imeenda kinyume kabisa na tulivyokubaliana, si mmeona hapa jamani?,” alisema Kikwete akihoji na kuongeza:

“Sisi huwa hatujengi eneo hili, ni udongo wa mfinyanzi mkali ambao wakati wa mvua ni tope na wakati wa kiangazi ni jiwe, hebu angalieni bwana.”

Source: Mwananchi Newspaper

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...