12 April, 2012

KABURI LA KANUMBA LAGHARIMU SH1.55MIL

MAANDALIZI ya kuchimba hadi kukamilika ujenzi wa kaburi alilozikwa aliyekuwa nguli wa tasnia ya filamu nchini, marehemu Steven Kanumba yamegharimu Sh1.55mil.

Kanumba alizikwa juzi kwenye makaburi ya Kinondoni baada ya kufariki mwishoni mwa wiki nyumbani kwake Sinza Vatican Dar es Salaam kwa kile madaktari walichodai ni kutokana na matatizo ya brain concession.

Habari za uhakika kutoka katika chanzo chetu cha habari zilizoifikia gazeti hili zilieleza kuwa kaburi hilo lililojengwa na Ofisi ya Utamaduni Wilaya Kinondoni kwa siku mbili kabla ya siku ya mazishi na kugharimu kiasi hicho cha fedha hadi kukamilika kwake.

Mwananchi iliyokuwepo makaburini hapo mapema juzi asubuhi kabla ya shughuli za mazishi, ilishuhudia wahusika 'wakipiga kazi' kuliwekea marumaru kwa ndani na sehemu kubwa lilikuwa limekamilika.

Hata hivyo, wahusika waliokuwepo hapo, hawakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kudai kuwa wao kazi yao kujenga na masuala mengine hawayafahamu.

Kilieleza kuwa tulianza kuchimba majuzi mchana na kujengea matofali na kufatiwa na zoezi la kujengea matofali kwa muda wa siku mbili na baada ya hapo tulimalizia kwa kuweka marumaru na ikawa tayari ujenzi umekamilika.  
 "Hii ndio gharama halisi ya matengenezo ya kaburi la Kanumba risiti hii hapa watu wanaweza kuongea mengi lakini ukweli ni huu," kilisema chanzo hicho cha habari huku kikionyesha risiti hiyo ya malipo ya shughuli nzima.

1 comment:

  1. hata kama imetumia kiasi hicho ninyi kinawahusu nini?

    ReplyDelete

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...