28 May, 2012

NILIPOKUTANA NA RAFIKI ZANGU WA FACE BOOK ANA KWA ANA




Picha ya kwanza:   Viongozi wa muda wa WAMO,
Picha ya pili:          Watoa mada 
Picha ya tatu:         Sehemu ya wanaharakati waliojitokeza katika mkutano wa kwanza wa
                               WAMO        
Picha ya nne:          Wanawake wawili  ‘WASHOKA’  JoJoTheFighter  na  Mamamia Mango
                               mara baada ya kuchaguliwa  kuwa viongozi wa WAMO

Mkutano wa WAMO ulifanyika Jumapili Tar 27 May 2012
MUDA: saa 8 mchana hadi saa 12 jioni.
MAHALI: UBUNGO PLAZA Dar es salaam.
WAHUSIKA: Yeyote mwenye NIA ya mabadiliko.
HAKUKUWA NA  KIINGILIO....
RATIBA.
1.Kuingia ukumbini
2.Kujitambulisha.
3.Kupitisha uongozi wa muda
4.Ufunguzi wa Mkutano na AGENDA

AGENDA ZA SIKU HIYO ZILIKUWA KATIKA MFUMO WA TOFAUTI 

 *** Zilikuwa katika mfumo wa maswali yaliyoandaliwa na katika kujibu yalizaliwa maswali mengine kutoka kwa wageni waalikwa.

AGENDA. 01.
Elimu ya darasani pekee yatosha kukuwezesha kulikwepa tatizo la ajira Tanzania???
MUHUSIKA. Shukrani Mbiligenda..Lect. Udsm/ Nobat na Mushobozi Udsm.

AGENDA. 02.
Kipaji chako chaweza vipi kukuajiri? Na kwa nini wenye vipaji wanalala njaa??
MUHUSIKA. Malle Marxist...Msanii wa Hip hop na mwanafunzi Chuo cha ustawi wa jamii pia mwandishi wa kujitegemea.

AGENDA 03.
Serikali/vyama vya siasa vinalitazama vipi suala la tatizo la ajira??
MUHUSIKA: Josephine Joseph, (JoJo The Fighter) msanii wa filamu, blogger, mhitimu chuo cha Tumaini, kiongozi wa CCM Kinondoni.

AGENDA 04.
Nani alaumiwe tatizo la ajira Tanzania???
MUHUSIKA. Christina Elisha Prosper...mwanafunzi S.U.A. Morogoro

AGENDA 05.
Usemi huu wa ' ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA', kama ni ufunguo wa maisha mbona walioipata hiyo elimu bado maisha yanawawia magumu??
MUHUSIKA. Adella Dally Kavishe....Mtangazaji Passion Fm, mwandishi wa vitabu.

AGENDA 06.
Kama kupata ajira Tanzania ni lazima uwe na cheti.....wale ambao hawakusoma nani atawaajiri?? kama hawajaajiriwa watajikimu vipi maisha yao???
MUHUSIKA. Deus Malya....Mwanaharakati, mfanyabiashara na mwanasiasa.

AGENDA 07.
Vijana wanaichukuliaje changamoto ya tatizo hili la ajira.
WAHUSIKA. Veronika Temba na mume wake.

AGENDA 08.
Ualimu na uaskari yamekuwa makimbilio kwa wale wasiokuwa na ajira. Je kimbilio hili ni sahihi???
WAHUSIKA. Fredrick Boniphace. Mwanafunzi chuo cha ualimu Kigurunyembe Morogoro.

AGENDA 09.
Maisha yanasemekana kuwa hayana ramani, kwa hiyo ni bahati nasibu kwa hiyo tungojee bahati kufanikiwa ama kushindwa katika mipango yetu. JADILI.
MUHUSIKA. Kalisti Mujuni. Mwalimu, mwandishi wa vitabu vya kiada na ziada, Mwanaharakati.

AGENDA. 10.
Kinyume na nchi za wenzetu, wenye vipaji wanaheshimiwa na kuwa nembo ya taifa, mbona Tanzania si hivyo???
MUHUSIKA. Beka Mfaume. Mwandishi mkongwe wa riwaya Afrika mashariki./ Lema raisi wa ASASI ya SAVE MY TALENT!!!! TANZANIA

AGENDA 11.
Vijana tumechukua hatua gani baada ya kugundua kuwa ukosefu wa ajira ni janga la taifa zima.
WAHUSIKA. Viongozi wa wapuuzi Movement.

BAADA YA HAPO ZILIKUWEPO AGENDA NYINGINE.
1. Kupitisha/kukataa jina la Wapuuzi Movement.
2. Majukumu ya uongozi wa muda
3.Historia ya chimbuko la Idea hii.
4. Mengineyo.
5.Kufunga na kupiga picha za ukumbusho!!!



 
 Tuliwa wakilisha vyema Wapuuzi wenzetu katika Studioa ya Passion F siku chache baada ya mkutano uliofanyika Ubungo Plaza....Watanzania walitusikia 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...