04 July, 2012

Mbunge aangusha kilio MJENGONI!


Bunge la jamhuri ya muungano jana lilijikuta likiwa kimyaaaaa kwa takriban dk 5  hivi wakati mbunge wa Viti Maalum, Al-shaymaa Kweigyir (CCM), alipoangua kilio cha kutisha mjengoni akilalamikia kukithiri vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Al-shaymaa huku akiitupia lawama Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaohusika na mauaji hayo alisema........“Inasikitisha jamani, Serikali imeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watu ambao wanawaua albino bila hatia….wamekuwa wakiwaua albino wasiokuwa na hatia mpaka sasa idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 80 nchini kote.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ndiyo mtu wa kutusaidia sisi walemavu wa ngozi, lakini umekaa kimya, hivi karibuni aliuawa faru ajulikanaye kwa jina la George na watu waliohusika na mauji hayo walikamatwa, kwa nini wauaji wa maalbino hawakamatwi.

“Hivi karibuni ameuawa albino huko wilayani Arumeru, hata alipogundulika kuwa ameuawa tayari alikutwa amekatwa viungo mbalimbali mwilini, ikiwemo sehemu za siri, kwa hali hii siungi mkono hotuba hii ya Waziri Mkuu, hadi nipate majibu,” alisema huku akihoji Mbunge huyo.

Hata hivyo, mbunge huyo alishindwa kujizuia na kujikuta muda wote, akibubujikwa na machozi, hali iliyomfanya ashindwe kuendelea, huku Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, akimbembeleza na kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...