02 October, 2012

Rais Obama dhidi ya Ufunuo 13:15-18

MWISHO UMEKARIBIA
Bunge au Seneti ya Marekani imepitisha mswada wa afya wa Obama kuwa sheria na utaanza kutumika tarehe 13/03/2013. Mswada huu utawataka Waamerika wote kupandikizwa chip yaani kifaa (kibanzi/upapi) kinachotumia mionzi ya redio kwa utambulisho (Radio Frequency Identification-RFID) ili kuweza kupata huduma za afya. Kifaa hiki kitapandikizwa kwenye paji la uso au mkononi.

Hii ni kutimiza unabii uliopo katika Kitabu cha Ufunuo 13:15-18 unaohusu CHAPA YA MNYAMA! Je, bado una mashaka kuhusiana na siku za mwisho? JIANDAE!
Unyakuo umekaribia! Uwe tayari usije ukakutwa hujajiandaa. Ishi maisha yaliyo safi. omba zaidi, hubiri INJILI kwa wengine ili uokoe roho zao. Ufunuo 13 unatimia mbele ya macho yetu. Wengi bado hawajalitambua hilo. 

1. Kwa nini hicho kifaa kinapandikizwa pale pale ambapo Biblia inataja kitakuwepo? Kwa nini    mkononi na kwenye paji la uso? Kwa nini siyo mahali pengine  popote?

2. Kwa nini kinaunganishwa na akaunti yako ya benki? 
Kumbuka Biblia inasema hutakuwa na uwezo wa kununua au kuuza kama huna hiyo chapa. Na Je, unafahamu! Kifaa hicho kinaunganishwa na taarifa zako zote zinazohusiana na pesa? 

Kinachouma moyo wangu kuliko yote ni kwamba watu wengi waliopo kanisani / misikitini hawatanyakuliwa iwapo Yesu atarud sasa.  Wengi hawajui kwamba wakati umekaribia.

Wala usiniambie kwamba haya ni maendeleo tu ya kiulimwengu, au teknolojia tu, au kitu cha kufikirika tu kama ndoto. 

Kama kuna eneo lolote katika maisha yako ambalo haliko sawa na neno la Mungu, ni wakati muafaka kugeuka kabisa haraka na kumrudia Mungu, tubu na jiandae maana mwisho umekaribia sana  ...Jehanamu siyo mahali pazuri kabisa, na ukweli ni kwamba ni mateso ya milele...tafadhali, jiunge nami kupiga mbiu hii. Mjulishe kila mtu unaye mfahamu....

TAFADHALI fanya sehemu yako katika hili.


UFUNUO 13:15-18 
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudia sanamu ya mnyama wauawe. 16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. 


Je, sisi tuyadharau mambo haya? na tunatakiwa kuitikia kwa namna ipi? Andiko kutoka ufunuo 13:15-18

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...