SHAHIDI wa tano katika kesi ya kutorosha wanafunzi inayomkabili
Mchungaji wa Kanisa la TAG, raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo
(DRC), Jean Felix Bamana ameieleza mahakama namna alivyolazimishwa
kufanya mapenzi na mchungaji huyo.
Shahidi huyo, Angela Swai (19), akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu,
Naomi Mwerinde wa Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, alisema Mchungaji
huyo alimlazimisha kufanya kitendo hicho jaribio ambalo lilishindikana
kutokana na mshitakiwa huyo kukataa kutumia kondomu.
Akiongozwa na mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Esther
Majaliwa, katika ushahidi wake, Shahidi huyo alieleza Mahakama hiyo
alivyokutana na mshtakiwa kwa mara ya kwanza na mara ya pili ambapo
alisema alikutana naye kupitia marehemu mama yake mzazi huku mara ya
pili akikutana naye kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Shahidi huyo alieleza mahakamani hapo kuwa alikutana na mshtakiwa kwa
mara ya kwanza kupitia mama yake na alimtambulisha yeye na mdogo wake
aliyemtaja kwa jina la Arthur kuwa mchungaji huyo ni baba yao mwingine
na waliendelea kufahamiana kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa mama na
mshirika wake katika Biashara ya Madini.
Alisema kwa kipindi kirefu hakuwahi kumuona hadi alipokutana naye kwa
mara ya pili mwaka jana kupitia mtandao wa Facebook ambapo alimwomba
urafiki kwa nia njema kwani alikuwa ni rafiki mkubwa wa marehemu mama
yake, na kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa ni ya kawaida tu.
Shahidi huyo alisema baada ya hapo mshtakiwa alianza kumsisitiza
kuhamia Dar es Salaam kwa ahadi ya kumsaidia kuendelea na masomo baada
ya kumueleza amefukuzwa shule jambo ambalo yeye binafsi alilikataa.
Alisema baada ya kukataa kukubaliana na wazo la kwenda Dar es Salaam,
mshtakiwa huyo alimwambia atafika Moshi ambapo alifikia katika Hoteli
ya Moshi View, Februari 14, mwaka huu na kufanya naye mawasiliano
kupitia simu ya mdogo wake aliyetajwa mahakamani hapo kwa jina la Arthur
Swai, akimtaka kumfuata hotelini hapo.
Chanzo: talkbongo

No comments:
Post a Comment