Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana ameanika majina ya watu
saba waliohusika kupitisha mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za
kulevya zenye thamani ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama
wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa
kutumia mbwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, lakini siku ya tukio hilo
mbwa hao walichelewa na walitumika baada ya mizigo kuingizwa kwenye
masanduku ya chuma.
“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi makubwa tisa yanayofanana si kitu cha
kawaida kukwepa jicho la maofisa wa ushuru wa forodha na vyombo vya
usalama, sijui walikuwa wapi siku hiyo?” alihoji Mwakyembe.
Juzi waziri huyo aliahidi kuyaweka hadharani majina ya watu
wanaosafirisha dawa za kulevya nchini, na alitekeleza ahadi hiyo jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari, kusema kuwa watu hao
wamenaswa baada ya mfumo wa kamera (CCTV) za uwanja huo kudaka matukio
kadhaa yaliyotokea siku ya tukio hilo, kuanzia saa 9:25 hadi saa 10:30
alfajiri.
Ameagiza wafanyakazi hao wanne pamoja na askari polisi mwenye cheo cha
koplo, mbeba mizigo na mfanyabiashara aliyekuwa na wasichana wawili
waliokamatwa Afrika Kusini, (ambao hatuwezi kuwataja kutokana na
kushindwa kuwapata kujieleza) kuchukuliwa hatua za kinidhamu, kukamatwa
na kuunganishwa na watuhumiwa waliokwenda na mzigo huo Afrika Kusini.
Mabegi hayo yaliyokuwa na dawa za kulevya aina ya ‘Crystal
Methamphetamine’, yalipitishwa na wasichana wawili wasanii aliowataja
kuwa ni Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward ambao walidakwa siku
hiyohiyo katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika Kusini na tayari
wameshafikishwa mahakamani.
Juzi Dk Mwakyembe alifanya ziara JNIA kukagua utendaji kazi kwenye
uwanja huo ikiwa ni siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza
kwamba katika kipindi cha wiki mbili, atahakikisha anawakamata vigogo
wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za
kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini.
Saa nane baada ya ziara hiyo, Maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
wanadaiwa kumkamata Edwin Monyo akiwa na kete 86 za dawa aina ya heroini
na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia
Zurich.
Mpango ulivyosukwa
Alisema siku ya tukio saa 9:28 kamera hizo za usalama zilimwonyesha
mbeba mizigo wa uwanja huo akiwa anazungukazunguka eneo la kuingilia
abiria kama mtu ambaye ana ahadi na kukutana na mtu fulani.
“Kamera pia zilimnasa ofisa mwingine wa TAA kwa mara kadhaa akitoka na
kuingia ndani ya jengo la abiria huku akizungumza na simu, kitendo
ambacho hakiruhusiwi kabisa kwa wafanyakazi wa eneo la ukaguzi wa
abiria,” alisema na kuongeza;
“Wakati huohuo, kamera zilikuwa zinamwonyesha askari polisi
anayetuhumiwa kuhusika katika mpango huo akiwa anarandaranda eneo la
uhakiki wa hati za kusafiria kama vile anasubiri kitu fulani.”
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...

No comments:
Post a Comment