RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete, ameingilia kati sakata la Mtume na Nabii Josephat Mwingira kudaiwa
kuzaa na mke wa mtu.
JK, aliingilia
kati sakata hilo baada ya mume wa mtu, Dk. William T. Morris, kukamatwa na
maofisa wa uhamiaji kisha kutakiwa kufukuzwa nchini kutokana na kile kinachodaiwa
ni ‘shinikizo la mtu mwenye nguvu’.
Habari ambazo zimezithibitishwa ni kwamba baada ya Dk. Morris kufungua mashtaka akimtuhumu
Mwingira kuzaa na mkewe, Dk. Philis Nyimbi, alikamatwa na maofisa wa uhamiaji
kisha kupewa hati ya kutimuliwa nchini.
Imebainika
kuwa JK ndiye
aliyezuia hati hiyo na mpaka sasa, Dk. Morris, raia wa Liberia, yupo nchini
akiendelea na harakati zake za kusaka haki kisheria kuhusiana na madai yake
hayo.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete.
JK
ALIMFIKIAJE?
Inaelezwa kuwa wakati Dk. Morris alipokamatwa, alitokea msamaria mwema anayejua
‘njia za kupita’ kufika Ikulu ambaye alimfikishia JK mkanda mzima wa sakata
hilo la Mwingira.“… (anataja jina la msamaria mwema), alimwambia JK kuwa nchi
inaelekea katika aibu, Dk. Morris ni mtu anayetambulika Umoja wa Mataifa (UN)
hasahasa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“JK baada ya kusimuliwa kila kitu, alichokifanya ni kuingilia kati na kuzuia
Dk. Morris asifukuzwe nchini,” kilisema chanzo na kuongeza:
Mtume
na Nabii Josephat Mwingira.
“Vilevile
JK aliomba namba ya Dk. Morris kisha alimtumia SMS na baadaye wakaongea,
akamhakikishia yupo salama nchini lakini kuhusu madai yake kuhusu mkewe,
aendelee kufuata sheria.”
HATI YAKE BADO INASHIKILIWA NA UHAMIAJI
Habari zaidi zinaweka kweupe pamoja na JK kuzuia Dk. Morris asitimuliwe nchini,
bado maofisa wa uhamiaji Mkoa wa Pwani, wanashikilia hati yake ya kusafiria
(passport) mpaka leo.
Dk. Morris alipoulizwa kuhusu hilo, alikiri: “Ni kweli
wanaishikilia. Niliwaomba wale maofisa wanipe nyaraka inayoonesha passport
yangu wanaishikilia. Niliogopa wanaweza kunigeuka. Waliniandikia, kwa hiyo sina
wasiwasi.”

Cheti
cha ndoa ya Dk. Morris na mkewe Dk. Philis.
MKANDA
MZIMA ULIANZA HIVI:
Gazeti pendwa lenye umiliki wa Global publishers liliandika habari yenye kichwa Mume: Mwingira amezaa na mke
wangu.
Katika habari hiyo, gazeti hilo
lilisimamia tuhuma zilizofunguliwa na Dk. Morris kwenye Kituo cha Polisi Kati
(Central), Kibaha, Pwani, akidai Mwingira amezaa na mkewe.
Shauri hilo lilifunguliwa kwa kichwa JALADA LA UCHUNGUZI,
nambari KBA/PE/20/2011, mtuhumiwa akiwa Josephat Mwingira.
Mke wa Dk. Morris, Dk. Philis, alidai
alizaa nje ya ndoa baada ya kutekelezwa na mumewe, ingawa alikataa kumtaja
mwanaume aliyezaa naye.
Zaidi ya hapo, Dk. Philis alisema Dk. Morris hakuwa mwaminifu
kwenye ndoa, kwani alidiriki kumsaliti kwa binti mwenye umri chini ya miaka 18
ambaye wao kama mke na mume, wangeweza kumzaa.
Mtoto wa Nabii Mwingira aliyezaa na Dk. Philis.
Katika kumchimba zaidi Dk. Morris, mwandishi alifanya naye
mahojiano kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Ni kweli ulimtelekeza mkeo ndiyo maana akaamua kusaliti na kuzaa nje
ya ndoa?
DK. MORRIS: Si kweli hata kidogo, amenisingizia, naomba amuogope Mungu.
MWANDISHI: Una ushahidi wowote kuwa ulikuwa unamjali mkeo?
DK. MORRIS: Ushahidi upo wa kutosha. Anazungumzia kipindi cha
kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, ni kipindi ambacho nilikuwa naishi Marekani
kikazi WHO.
Kipindi hicho, nilikuwa namtumia mke wangu dola za Kimarekani 2500 (zaidi ya
shilingi 4,000,000) kila baada ya wiki mbili lakini kuna wakati nilikuwa nampa
zaidi ya hizo.
Mwandishi
alioneshwa nakala ya karatasi za kibenki zikionesha
jinsi alivyokuwa akimuingizia fedha mkewe aliyekuwa na akaunti katika Benki ya
Standard Chartered Moshi (namba ya akaunti tunaihifadhi), yeye akiwa Marekani
akitumia Bank of America kuanzia mwaka 2006.
MWANDISHI: Hebu niambie, Dk Philis bado ni mke wako? Yeye
anasema wewe siyo mumewe.
DK. MORRIS: Ni mke wangu halali wa ndoa takatifu. Nilifunga naye ndoa katika
Kanisa la St Alban, Dar Desemba 23, 2001, nikiwa na umri wa miaka 39 na yeye
(mkewe) akiwa na miaka 30.
Ndoa hiyo niliigharamia sana tangu mavazi ya wapambe wangu na
wa mke wangu. Ilikuwa siku ya furaha kabisa. Sikupenda wakwe zangu wapate
shida.
MWANDISHI: Ukiwa Marekani ulipata habari zozote za kuwa mkeo ni mjamzito au
kajifungua?
DK. MORRIS: Hapana, sikuwa na habari kabisa juu ya jambo hilo
na ndiyo maana nilikuwa nikimtumia fedha za kutosha.
Kuna siku moja aliniambia anataka kwenda kufanya utafiti Afrika Kusini,
akawa anataka dola 2500 siku hiyohiyo aliyoniambia. Nilimwambia taratibu
za fedha Marekani ni ngumu. Nilikwenda ofisini kwangu nikaomba malipo ya awali
ya mshahara wangu, nikamtumia dola za Kimarekani 3,000 (shilingi milioni 4.8
kwa chenji ya sasa).
MWANDISHI: Uliporejea Tanzania, ilikuwaje ukajua mkeo amezaa
nje ya ndoa?
DK. MORRIS: Nakumbuka usiku mke wangu alianza kulia. Nilishangaa nikamuuliza
kwa nini unalia, akanijibu kwamba anaomba nimsamehe kwa sababu amezaa nje ya
ndoa.
MWANDISHI: Baada ya kusikia hivyo ulijisikiaje?
DK. MORRIS: Niliishiwa nguvu kabisa, nikamuuliza kwa nini
amefanya usaliti huo? Nilimuuliza ni nani amempa mimba, akaniambia ni mwanaume
mmoja injinia ambaye alidai yupo Marekani kwa wakati huo.
MWANDISHI: Hayo ulikuwa unamuuliza mkiwa wapi Dar au Kibaha?
DK. MORRIS: Tulikuwa Moshi, nikiwa Marekani mke wangu
aliniambia yupo Moshi anachukua shahada ya pili (Master) ya udaktari, na
nilikuwa namtumia fedha za pango la nyumba, lakini pale nilimkuta hotelini,
kesho yake tukarudi Dar.
MWANDISHI: Baada ya kufika Dar mambo yalikuwaje?
DK. MORRIS: Mke wangu aliniambia kuwa ni lazima nimsindikize kwa Nabii Mwingira
ili akaombewe kwa ushetani alioufanya wa kuzaa nje ya ndoa.
MWANDISHI: Ulikubaliana naye?
DK. MORRIS: Nilimkubalia tukaenda kwa sababu wakati huo nilikuwa sijajua kuwa
yeye ndiye mbaya wangu. Tulimkuta na akatukaribisha ofisini kwake.
MWANDISHI: Mambo yakawaje?
DK. MORRIS: Mwingira alituombea, wakati akituombea Mwingira
mwenyewe alilia sana.
MWANDISHI: Ukaja kumtuhumu vipi tena Mwingira kuwa amezaa na mkeo?
DK. MORRIS: Subiri kwanza, kesi ikishakuwa mahakamani yote yatakuwa wazi.
Nitataka pia tupimwe kila kitu, DNA pamoja na Ukimwi.
MWANDISHI: Vipi madai ya wewe kutimuliwa nchini?
DK. MORRIS: Namshukuru sana Rais Kikwete, ni kiongozi mzuri, alinisaidia sana.
Namuamini, nampenda na nawaomba Watanzania wampende kiongozi huyu, ni mpenda
haki.
MWINGIRA BADO SHIDA
Jitihada za waandishi wetu kumpata Mwingira bado hazijazaa matunda, kwani kila
njia inayotumika, wasaidizi wake hawataki kabisa kiongozi huyo wa Kanisa la
Efatha, afikiwe na kuhojiwa kuhusu madai haya.
Hata hivyo, waandishi bado hawajakata
tamaa, wataendelea kumsaka mpaka apatikane
na kujibu tuhuma hizo.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment