14 January, 2014

SAFARI YA MWISHO YA AIRIEL SHARON

Watu nchini Israel wapo katika kipindi cha maombolezi kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani Ariel Sharon aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya miaka 8 ya kuwa hali mahututi.
Viongozi wa dunia wametoa rambi rambi zao kwa Sharon, mtu aliyepigana katika vitaa vikuu vinne kabla ya kuingia katika ulingo wa siasa.
Lakini aliwaacha wapalestina wengi waliomuona kama adui wao wakiwa na hamaki.
Mkuu wa kituo cha afya cha Sheba mjini Tel Aviv alithibitisha kifo cha Sharon, Jumamosi mchana siku ya Sabato kwa wayahudi, zaidi ya wiki moja baada ya taarifa kutolewa kuhusu afya yake kuzorota.
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea kuwahudumia watu wa Israel.
Rais Shimon Peres, mwandani mkuu wa Sharon japo alikuwa hasimu wake wa kisiasa aliyejiunga na serikali ya Muungano na Sharon mwaka 2001, alisema Sharon alikuwa mtu mwema aliyepigania watu wake na kuwapenda na kuwa watu pia walimpenda.
Wadhifa wa Sharon kama waziri mkuu ulifika kikomo baada ya kupatwa na kiharusi na kisha kuwa katika hali mahututi kwa miaka minane tangu mwaka 2006.
Wakati huu wote alikuwa anatumia mashine kupumua na mirija kulishwa chakula.
Kabla ya hali ya Sharon kuzorota aliongoza jeshi la Israel kuondoka katika ukanda wa Gaza ili kupunguza taharuki kati ya Israel na Palestina.

Wananchi wa Israel jana Jumatatu 13/01/2014 wametoa heshima zao za mwisho kwa Waziri Mkuu wa zamani Ariel Sharon mtu ambaye amesifiwa kuwa ni shujaa wa vita nchini mwake na kuonekana kuwa mhalifu wa vita na nchi za Kiarabu. Wananchi wa Israel leo wametowa heshima zao za mwisho kwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ariel Sharon katika ibada mbili za mazishi kwa mtu ambaye amesifiwa kuwa ni shujaa wa vita nchini mwake na kuonekana kuwa ni mhalifu wa vita kwa ulimwengu wa Kiarabu.
Makamo wa Rais wa Marekani John Biden na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steimeir ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria ibada ya mazishi mbele ya bunge la Israel wakati jeneza la Sharon lililofunikwa bendera ya Israel likiwa limewekwa uwanjani.
Akiwasilisha rambi rambi zake Biden amesema Sharon alikuwa ni mtu ambaye nyota iliokuwa ikimuongoza ilikuwa ni usalama na uhai wa taifa la Israel.Biden amesema kwa ushujaa mkubwa Sharon katu,katu,katu hakuyumba kwenye lengo hilo.
Rais Shimon Perez wa Israel naye amesema leo wanamsindikiza kwenye mapumziko yake ya milele mwanajeshi,mwanajeshi wa aina yake,kamanda ambaye alikuwa akijuwa namna ya kupata ushindi.
Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 hapo Jumamosi baada ya kupoteza fahamu kwa miaka minane kulikosababishwa na kiharusi
(Chanzo BBC)

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...