THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni
Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete
ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania
na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa
na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume
yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya
Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa
Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko
Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi
kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea
miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho,
Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public
Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar
ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Mwisho.
Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
Dar es Salaam.
12 January, 2014
No comments:
Post a Comment