Wenyeviti wa CCM mikoa ya Tanzania
bara wametoa tamko la kumkana Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti CCM Taifa Mgana
Mzindakayi la kutowauza wenyeviti wenzake kwa watu wanaotarajia kugombea
urais kabla ya muda na utaratibu wa Chama kufika.
Hatua hiyo inafuatia tamko
lililotolewa kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Tanzania bara Joseph
Msukuma leo jijini Mwanza kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msindayii
ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida alipoalikwa kwenye sherehe ya
kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya wilayani Monduli
Kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na
Mjumbe wa NEC na mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambapo katika salamu zake
Msindayi alinukuliwa na vyombo vya habari na taarifa zake kutoka leo
akisema kuwa yeye pamoja na wenyeviti wa CCM wa mikoa yote nchini wako nyuma ya
Lowassa wakimuunga mkono kauli ambayo imewaweka katika wakati mgumu na
wenyeviti wa CCM mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kuanza kuwagawa na
kutengeneza makundi.
hiki ndicho walichokisema wenyeviti
Ccm Tanzania Bara 2014
No comments:
Post a Comment