28 February, 2014

MADIWANI WAWILI WA CHADEMA WAJIUZULU

Madiwani wawili wa CHADEMA Shinyanga wajiuzulu
Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa madiwani wawili wa Shinyanga wamejiuzulu, madiwani hao ni Sebastian peter kata ya Ngokolo na Zackaria Mfuko kata ya Masekelo.

Madiwani hao wamesema hoja yao ya msingi ya kufikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao ni kuwa wamechoshwa na siasa za chama chao ambazo zinalenga kutafuta umaruufu kuliko kuimarisha chama, na siasa za kujenga na kuimarisha makundi ambayo yanaasisiwa na viongozi wakuu na ndio wachochezi wa mkawanyiko ndani ya Chama.

HIVYO wameamua kujiuzulu nafasi zao kwa kuwa hawaoni future kwa Chama hicho wala hawaoni ukombozi wa kweli kwa wananchi kupitia Chama hicho
By Jini mahaba
Katika hali ya kuonyesha Uhai wa Chadema kuelekea 2015 ni kukatisha tamaa na kumpa hofu ya anaekiuguza chama hicho japo sio busara kumkataza mgonjwa anaekalibia kufa kunywa dawa na kumpa moyo atapona tuu japo moyoni unajua lazima afe Madiwani wawili wa chadema wameamua kujiuzulu Madiwani hao wanaojulikana kwa jina la

1.) ZACHARIA MFUKO Wa kata ya MASEKELO na

2.) SEBASTIANI PETER Wa kata ya NGOKORO

Sababu walizozitoa madiwani hao ni kushoshwa na uongozi kandamizi wa Freeman Mbowe na jopo lake huku wakiumizwa na siasa za chama zao za kutaka umaarufu kuliko kuwatumikia watanzania akiongea kwa jaziba SEBASTIANI PETER Wa kata ya NGOKORO "alisema Chadema inapoteza mvuto kwa watanzania hasa baada ya kutumia chopa tatu na milion mia tisa za chama hicho huku kikiambulia kata tatu tuu " lakini mpaka sasa hakuna kikao kilichoeleza na kufanya tathimini kwa nini chama kimepoteza kiasi hicho.

Aliendelea kusema mengi huku akisema yapo mengi yamewasukuma Kukikana chama hicho ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa mali za chama ruzuku kutumiwa na wachache, chama hicho kua na harufu ya ukabila na udini alizidi kusema na mengine mengi ambayo si busara saana kuyasema.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...