
Kufuatia
tukio la taarifa za awali kuhusu kupotea kwa ndege ya shirika la
Malaysia airlinesaina ya Boeing yenye namba 777 MH370 nchini Malaysia
kwa takribani siku 16 hadi sasa, hatimaye Waziri
mkuu wa Malaysia Bw. Najib Razak ametoa taarifa ya awali kuhusiana na ndege hiyo.
Ripoti
hiyo iliyosomwa na waziri huyo, inasema kuwa ndege hiyo ya Malaysia
airlines ilidondoka kusini mwa bahari ya Hindi huku ikielezwa kuwa hadi
sasa hakuna matumaini ya kupona kwa abiria waliokuwamo katika ndege
hiyo.
Ikumbukwe kuwa, ndege hiyo ilitaarifiwa kupotea tangu marchi 8 2014 ikitokea Kuala Lumpur huku ikiwa na jumla ya abiria 239.Na hadi sasa shughuli ya kuipata miili ya marehemu hao inaendelea kufanyika. Hivyo basi endelea kukaa karibu na www.msombe.blogspot.com kwa taarifa zaidi.
Hapa chini ni baadhi ya picha za wanandugu wakiomboleza kwa uchungu kufuatia tukio hilo.
No comments:
Post a Comment