Waziri mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu
Fredrick Tluway Sumaye amezindua kitabu kipya kabisa kiitwacho
Kufurahia ndoa ambacho kimeandikwa na mchungaji Zakayo na Carol Nzogere
wachungaji wa kanisa la Mwanza International Community Church katika
uzinduzi uliofanyika siku ya jumapili hii na kuhudhuriwa na mamia ya
wakazi wa jiji la Mwanza.
waziri
mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akikiangalia kitabu cha Kufunurahia
ndoa,kulia ni mchungaji Zakayo na Carol Nzogere wakifatilia kwa umakini
Katika kuzindua kitabu hicho Mh.Sumaye
ameelezea kua Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa waandishi wa vitabu
kama mchungaji Zakayo na Carol Nzogere na waandishi wengine wengi zaidi
ambao watafanyika kua chachu ya maendeleo na kutatua matatizo mengi
kupitia kuyaweka mawazo yao katika maandishi picha au kumbukumbu ya kile
kilichowahi kuwatokea ili yaweze kuwasaidia na kutoa manufaa kwa watu
wengine watakaosoma mawazo hayo katika vitabu.
Aidha Sumaye amewapongeza Mchungaji
Zakayo na Carol Nzogere kwa kuweza kutumia muda wao na maarifa yao
katika kuandika kitabu hiki ambacho kinaeleza wanandoa wafanye nini ili
ndoa zao zipate kuwa imara na pia kuweza kutatua tatizo linalokua siku
hadi siku hadi siku katika taifa, tatizo la ndoa nyingi kutetereka hadi
kuvunjika na kupelekea kutokea kwa matatizo kama chuki baina ya waliokua
wana ndoa, maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wanandoa pale ambapo
wanandoa huanza kukomoana kwa kuanza michepuko nje ya ndoa.
Kufurahia ndoa ni kitabu ambacho
kimeandikwa na Mchungaji Zakayo na Carol Nzogere, wachungaji na wanandoa
ambao wamepata kudumu katika ndoa yao kwa miaka 14 sasa ,kitabu ambacho
kimebeba maudhui ya masuala ya ndoa kwa ujumla kikiwa na mafundisho juu
ya namna ya kuiboresha ndoa kwa watu waliopo ndani ya ndoa na wengine
ambao wapo katika mchakato wa kufunga ndoa hivi karibuni ili waweze
kupata maarifa namna gani ya kuzifanya ndoa zao ziwe zenye furaha na
amani tele katika maisha yao yote.
No comments:
Post a Comment