22 April, 2014

MCHEZAJI GABON AFARIKI UWANJANI



Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke la kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.
Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambako ni umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...