
Amesema amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa
shughuli zake mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo na
ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha (U T U)
inafanya vizuri zaidi na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa
karibu sana wa shughuli za umoja huo.
Mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo
alithibitisha safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U
T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa
bahati mbaya haikuwezekana kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao
ingawa UTU ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii
wa Tanzania.
U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.
No comments:
Post a Comment