Dar/Arusha. Jeshi la Polisi Zanzibar limeendelea kuuchelewesha mkutano
wa wanachama wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa madai
kwamba hakuna askari wa kutosha kuulinda.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema mkutano huo utafanyika leo katika uwanja huo. PICHA|MAKTABA
Awali, mkutano huo ulipangwa kufanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Kibandamaiti, Unguja lakini jeshi hilo liliuzuia kwa madai ya kuwapo kwa habari za kiintelijensia dhidi ya tishio la maisha ya watu.
Awali, mkutano huo ulipangwa kufanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Kibandamaiti, Unguja lakini jeshi hilo liliuzuia kwa madai ya kuwapo kwa habari za kiintelijensia dhidi ya tishio la maisha ya watu.
Awali, Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema mkutano huo utafanyika leo katika uwanja huo.
Ukawa ni muungano wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, DP na wajumbe
25 kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina alisema baadaye kuwa mkutano huo hautafanyika hadi Aprili 30, mwaka huu.
Alisema umezuiwa kwa sababu askari na maofisa wa polisi wanaotakiwa
kuusimamia wako Dar es Salaam katika maandalizi ya sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Tumekutana nao (CUF walioomba kibali kwa niaba ya Ukawa) na kukubaliana
kwamba mkutano huo ufanyike Aprili 30 kwani askari waliopo hivi sasa ni
wachache hawawezi kutosha kusimamia ulinzi kutokana na aina ya mkutano
wenyewe. Hata hiyo siku hiyo hakutakuwapo na maandamano, bali
wataruhusiwa kufanya mkutano pekee na siyo vinginevyo.”
No comments:
Post a Comment