MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA),
amewataka wakulima, wafugaji kuipiga mawe Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwa kutenga sh bilioni 50 kwa ajili ya safari za rais
huku ikitenga sh bilioni 51 kwa maendeleo ya kilimo.
Akichangia
hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Mdee alisema
serikali haina nia ya dhati ya kuutokomeza umasikini, ikiwemo
kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi.
Alibainisha
kuwa katika bajeti ya mwaka jana, serikali iliahidi asilimia 10 ya
bajeti itakwenda kwenye kilimo, lakini ikaishia kutenga asilimia nne, na
bajeti ya mwaka 2014/2015 imetenga sh bilioni 51 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo ya kilimo.
Alisema
kiwango hicho kimepishana kidogo na kile kilichotengwa kwa ajili ya
safari za Rais Jakaya Kikwete, ambazo zimetengewa sh bilioni 50.
“Wakulima,
wafugaji na wavuvi wanapaswa kuipiga mawe Serikali ya CCM, hapa
mmetuletea bajeti, lakini ukiangalia kwa kina utaiona haina dhamira ya
kuwasaidia wananchi,” alisema.
Mdee,
alisema bajeti ya Wizara ya Kilimo kila mara imekuwa ikitengewa fedha,
lakini hazifiki kwa walengwa, hivyo mipango mbalimbali imeshindwa
kutekelezeka.
Alisema
kuwa serikali kupeleka huduma kwa wananchi ni lazima na sio hiyari,
hivyo wabunge wa upinzani wanapokosoa utendaji wa serikali hawafanyi
jambo baya bali wanatekeleza wajibu wao.
Aliongeza
kuwa serikali kila mara imekuwa ikipewa ushauri mbalimbali, lakini
inashindwa kutekeleza jambo linalosababisha kukosa mapato yanayotakiwa.
Alisema
miaka minne iliyopita upinzani ulipendekeza kodi ya mishahara kwa
wafanyakazi ishuke chini ya asilimia 10, lakini serikali ilishindwa
kutekeleza jambo hilo hadi hivi sasa ilipoamua kushusha kutoka asilimia
13 hadi 12.
Aliongeza
kuwa Kamati ya Bajeti inafanya kazi kwa niaba ya Bunge na imelalamika
inatoa mapendekezo serikalini lakini inapuuzwa hali inayoonyesha
serikali haina dhamira ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato
visivyowaumiza wananchi.
Mkosamali amvaa Chenge
Mbunge
wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), aliituhumu Kamati ya
Bajeti kuwa inafanya vikao visivyo na tija ilimradi ihalalishe wajumbe
wake kupewa sh 500,000 kwa kila kikao.
Alisema
anashangazwa na kamati hiyo kuendelea kulalamikia kupuuzwa kwa ushauri
wanaoutoa kwa serikali wakati wana uwezo wa kutoa azimio la kukataa
bajeti hadi walichokishauri kifanyiwe kazi.
“Jamani
tuwe wakweli hapa, sisi tunalalamika tu wakati uwezo wa kubadilisha
mambo tunao, tukubaliane hapa kuikataa bajeti hii mpaka serikali
itakapoleta bajeti yenye tija kwa taifa.
“Kamati
ya mzee Chenge taarifa yao inalalamika kuanzia mwanzo mpaka mwisho
halafu inasema inaunga mkono bajeti, hivi kama si unafiki ni nini?
Inakaa hivi sasa na mashirika kujadili kuwapunguzia kodi… hii ni rushwa
tupu,” alisema.
Mbunge
wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema serikali imeshindwa
kutumia ushauri wa kuanzisha kituo cha uvuvi wa samaki katika bahari
kuu, ambako samaki wanavuliwa bila kulipiwa ushuru na kampuni kubwa.
“Nyinyi
serikali mna tatizo gani kila mwaka tunawapa ushauri na wataalamu wenu
wanaandika ripoti zinazoonyesha umuhimu wa kuanzia kituo cha uvuvi
katika bahari kuu, huko tunapoteza mapato mengi lakini hamjali, nyinyi
akili zenu zinawaza nini?” alihoji.
Mbunge
wa Kisarawe, Suleiman Jaffo (CCM), alisema kiwango cha asilimia
kilichopunguzwa kutoka katika kodi inayotozwa kwenye mishahara ni kidogo
na hakina msaada kwa wafanyakazi.
Alisema
serikali inapaswa kujikita zaidi kwenye kutafuta vyanzo vipya vya
mapato badala ya kila kukicha kuwabana wafanyakazi na wananchi.
No comments:
Post a Comment