24 June, 2014

MISTARI YA FID Q NA KISA CHA LADY JAY DEE

20140621-105223-39143149.jpg
“Today I Went Shopping… And Talk Still Cheap” ni maneno ya Lil Wayne kwenye moja ya nyimbo yake ya nyuma kidogo ijulikanayo kama “She Will” na msanii huyu naweza nikasema au kumpa wasifu kuwa ni “Rap Genius”
Lyrics ni mfumo mzuri sana wa muunganisho kati ya msanii na mashabiki sababu kila msanii ana utamkaji wake wa maneno katika style yake anavyoimba au anavyo Rap. Ni rahisi sana kwa mara ya kwanza msikilizaji akaweza kusikia nyimbo na kushika neno moja baada ya lingine, ili aweze kuimba na wewe na kujisikia kushiriki kikamilifu wakati nyimbo inapigwa au unaperform kwenye stage. Msikilizaji kuweza kupata mashairi (Lyrics) wakati nyimbo inatoka, ni rahisi sana kwa yeye kuweza kuimba na msanii mara chache huku akisoma mashairi na kuweza kuyashika kwa haraka sana.
Nimechukulia mfano wa mashairi ya Lil wayne “Today I went Shopping… And talk still cheap” sababu mara ya kwanza nilivyoisikia nyimbo hiyo, mara moja niliingia online na kuweza kufanya hivyo na baada ya hapo hiyo line ilinikaa kichwani muda mrefu sana na kuweza kutaka kuusikia tena na tena sababu inanisaidia sana na nakutana na vitu vingi vinavyomaanisha maneno hayo kama tunavyoelewa hapa duniani maneno yanayotoka midomoni kwa watu ni mengi sana kuliko vitendo ambapo maneno mengi ni “cheap” sababu utekelezaji wake ni mchache sana.
Kuna wasanii wengi sana wa kitanzania ambao wanafanya vizuri sana katika style zao za uandishi na jinsi wanavyoflow. Msanii kama Fid Q ni msanii ambae ni ngumu sana kumuandikia mashairi sababu ana uwezo wake binafsi wa kuelezea habari kwa njia yake yeye ambayo tokea ameanza kwa mashabiki wake na wasikilizaji wake kama mimi, humuelewa sana kutokea nyimbo zake za mwanzo. Msanii Fid Q ana Lugha gongana lakini upangiliaji wake wa lugha hiyo kama utamsikiliza kwa makini na tena ukiwa na Lyrics za nyimbo zake ni dakika chache tu utakua umemuelewa na utakua mwanachana wa “Sing Along” wa kila nyimbo anayopiga. Vile vile Lyrics zake hunifanya niweze kulinganisha au kufafanuloa vitu vibgi sana nnavyokutana navyo katika maisha ya kila siku.
“So usini’treat kama 2nd Class, utakua umefanya 1st Class Mistake” ni maneno ukiyasikiliza unaweza ukasema ni maneno tu lakini yana maana kubwa na yanachukua upeo mkubwa sana ukiyaweka katika uhalisia wa vitu vinavyotokea katika maisha yako ya kila siku kama ukizingatia na kuelewa Poet hiyo iliyotumika kutoka kwa mwana sanaa kama huyo. Sanaa hii hutumika hasa pale mtu anapoamua kukushusha kwa sababu zake lakini hajui Level yako ya maisha na hajui wewe ni nani lakini anaamua kuku’judge anavyojua yeye.
Sababu ya kukazania mstari huu unanikumbusha mbali kidogo miaka ya nyuma kidogo Msanii Lady Jay Dee akiwa na wenzake walienda Sheraton/Royal Palm/Movenpic na sasa ijulikanayo kama Dar Es Salaam SERENA Hotel akiwa na rafiki zake wa kike na pesa zao ambapo walikua wameenda kula bata kama wananchi wengine tu. Baada ya kufika Kibo Bar kuketi na kuagiza vinywaji ili kuendesha starehe zao ambazo uwezo wa kunywa mpaka wachoke bila kumbugudhi mtu. Msanii huyu na radiki zake baada ya kuagiza kinywaji, badala ya kuletewa kinywaji akaja manager   wa sehemu hiyo na kuwaambia kuwa hawaruhusiwi kukaa eneo hilo. Lady Jay Dee hakupendezewa na hicho kitu especially mtanzania mwenzake kuja na kuamua kumtoa sababu walikua ni wasichana peke yao na ile sehemu ni 5 Star Hotel kuwa na “foreigners” wengi ikaonekana kuwa wao pia wameenda “Hunting” ya wanaume…. Mistake, “Usini’treat kama 2nd Class, Utakua umefanya 1st Class Mistake”
Kitendo hichi hakikumfurahisha mtu yeyote ambae alipata nafasi ya kusikia maneno haya, sababu Lady Jay Dee ni msanii ambae anaheshimika na mwenye uwezo tokea kipindi hicho kuweza kuingia Hotel kubwa kama hiyo na kuweza kufanya matumizi yake, vile vile ni mwananchi ambae sheria inamlinda kuweza kuingia katika Hotel hiyo ma kufanya matumizi ya 1st class ambayo wao waliamua kumchukulia kuwa ni 2nd Class na haruhusiwi kuwepo pale na marafiki zake. Huu ni mfano mmoja tu kati ya mifano mingi sana ya watanzania ambao haki zetu zipo wazi laki watanzania wengine kwa madaraka yao wanaamua kufanya wananchi wengine katika nchi hii kuwa “2nd Class” na kuachiwa kuweza ku’get away with “1st Class Mistake” ambayo wanatakiwa kuhukumiwa juu ya kosa hilo walifanyalo. Mstari huu una maana kubwa sana kama ukizingatia na kuuelewa kutoka kwa msanii ambae ni mmoja wa wasanii ambao siku zote nawapaga TUZO zangu mimi binafsi naitambulisha ka “Lyrical MASTER” aka “Lyrical Genius” ambayo kwa sasa kuna wasanii 2 wa HIP HOP nchini Tanzania ambao binafsi nimewatunuku na siku zote hunikosha kwa mistari yao ambao na sijawahi kuacha kusikiliza kwa makini kila nyimbo wanazotoa au kufanya featuring, wasanii hao ni FID Q na MWANA FA ambao naweza nikasema nimekua nao kimuziki tokea wanaa

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...