Shughuli za Bunge zimesimama kwa muda baada ya umeme kukatika wakati upigaji wa kura kupitisha Bajeti ya serikali ukiendelea!!!!...
Hii ni fedheha na ni aibu ya karne kwa hii serikali na idara ya mambo ya Nishati ya Umeme.
Kitendo cha kuzimika umeme ni kitendo kisicho faa wala kukubalika kitaifa na kimataifa.
Nategemea yafuatayo yafanyike:
- Waziri wa nishati bwana Sospeter Muhongo na madini ajiuzulu kwani
amelifedhehesha na kuliaibisha taifa kwa wasimamizi wake kutokuwa makini
katika utekelezaji wa majukumu yao.
- Mkurugenzi mkuu wa TANESCO naye awajibike ili kuepusha hali hii iliyojitokeza katikati ya bajeti ya Taifa.
- Kiundwe kitengo maalumu cha usimamizi wa masuala ya umeme kwenye kumbi
na majengo makubwa na maalum ya kiserikali nchini ili waweze
kuhakikisha aibu kama hii haijirudii tena.
Ni ushauri tu, siyo amri.
No comments:
Post a Comment