09 September, 2014

IGUNGA WAKIRI MWIGILU NCHEMBA NI SOKOINE WA 11

Watu wa Igunga wakiri Mwigulu Nchemba ni SOKOINE wa II. Yeye asema tutaipeleka Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati 2015-2025.
Naibu waziri wa fedha aliyetokea kugusa mioyo ya watanzania masikini na kufufua matumaini yao ndg Mwigulu Nchemba juzi alikonga nyoyo za wananchi wa Tabora waliofurika Igunga kumsikiliza. Mwigulu aliyekuwa akishangiliwa kila alipofafanua  hoja aliwaacha wanaigunga wakibaki makundi makundi mpaka giza lilipoingia wangali viwanja vya Sokoine kutafakari hotuba yake iliyokuwa na sura ya kiongozi wa taifa. 
Katika hotuba yake mwigulu alirudiarudia neno "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI IFIKAPO 2025" na kushangiliwa kwa kishindo.
Mwigulu alibainisha kuwa mambo ya msingi kufikia hatua hiyo kuwa ni 
1) Maadili na uzalendo wa wasimamizi wa rasilimali za taifa. Mwigulu alisema wanahakikisha kwamba kila fedha inakwenda kutoa huduma iliyokusudiwa, tunahakikisha kodi za wananchi zinakwenda zilipokusudiwa. Tukikusanya fedha kwa ajili ya umeme, tunasimamia iende kwenye umeme, tukikusanya fedha ya barabara tunahakikisha zinakwenda kwenye barabara, hivyohivyo kwenye Afya, elimu nk. Mwaka jana tumegundua tulitoa zaidi ya 48bil kwa ajili ya dawa mawilayan lakkni ni 7bil zilitumika kununua dawa huku kila mgonjwa akienda hospital anahundulika na homa na kuambiwa kanunue dawa kiosk kile, huu ni wizi, kiosk kinatoa wapi dawa ambazo serikali haiwezi kupata kama sio kufanyia biashara dawa zilizonunuliwa kwa kodi za watanzania. Naagiza hili likome na hatua zitachukuliwa, madiwan na vyombo vya dola simamien hili. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"

2) Kuachana na kufanya kazi kwa mazoea. Mabadiliko ni vitendo na yanaonekana kwa kubadili style ya kufanya kazi ili kulinda fedha za umma. Timebadili ulipaji wa mishahara kipambana na mishahara hewa. Tumebaini zaidi ya wafanyakazi elfu kumi na nne (14,000) walioyeyuka tjlipoomba akaunt zao na 1,900 wa keshi nao wameondolewa kwenye malipo. Tumeokoa zaidi ya bilion 40. Naagiza maofisa wote wahakiki watimishi waliopo kazini na walete akaunt. Tukibaini makosa yule aliezembea atafute kazi ya kufanya na hatua zitachukuliwa. Mpk sasa waliozembea tumewapeleka polisi na TAKUKURU wafikishwe mahakamani.
Tumekagua madai tukagundua udanganyifu, kwenye bilion 500 tumegundua halali ni bilion m100 tu, tumeokoa bilion 400 na tumewapeleka polisi wote waliodanganya. Naagiza wakaguzi watimize wajibu wao kabla ya kuleta madai wizani kwangu. Wakileta tutskagua, Tukigundua udanganyifu aliyeleta hiyo atafute kazi nyingine ya kufanya na tutamburuza mahakamani. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"

3) Tutapunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho kwa kutekeleza vyema sera za kodi. Tutawatoza kodi matajiri ili fedha hizo tuwasomeshe watoto wa masikini. Tutatoza kodi matajiri ili fedha hizo tupeleke huduma za maji, madawa, umeme na barabara vijijini. Hatuwezi kuwasamehe kodi matajiri mabilioni ya shilingi, wakwepe mabilioni ya shilingi halafu sisi tukimbizane na wajane wanauza matembere kulipa ada elfu 20 mashuleni. Tumefuta misamaha kwa matajiri tuache kuwssumbua wajane na masikini kutafuta elfu 20 za sekondari. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"

4) Tutasimamia mgawanyo wa rasilimali ili keki ya Taifa iwanufaishe watanzania wote kwa usawa. Tumebana matumizi ya serikali yasio ya lazima ili fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo. Tutahakiki bajeti za kila taasisi ya umma na kufuta matumizi ya anasa. Hatuwezi kuwa na shirika la umma linatumia fedha kwa anasa huku watoto wakikaa chini. Kupewa kuvuna rasilimali za umma ni dhamana tu sio shamba binafsi na mashirika na taasisi zote za umma mnaokusanya fedha tokea rasilimali za Taifa mlielewe hili. Hatuwezi kuwa na watanzania hapa wanaishi tanzania na wengine wakiishi kama ulaya wakiwa hapahapa kisa wamepewa dhamana ya kusimamia shirika la umma. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"

5) Tutatoza kodi kwa matajiri, tuwapinguzie kodi walimu na wafanyakazi wengine, tutatoza kodi tuziwezeshe sekta zinazotoa maisha kwa watanzania wengi ili KUONDOA UHUSIANO WA KUKUA KWA UCHUMI HUKU UMASIKINI NAO UKIKUA. Tukiwedha fedha kwenye sekta zinazolisha na kuendesha maisha ya watu wengi tutakuza uchumi huku umasikini wa watu wa chini ukipungua.

6) Kuna watu walinunua viwanda vyetu, wamelipa, wamewekeza, wameendeleza, wametengeneza ajira, wameheshimu mikataba, wanalipa kodi nawapongeza sana. Lakini nimeangalia kumbukumbu kwenye mafaili kuna watu walinunua viwanda, hawajawekeza, hawajaviendeleza, wamegeuza viwanda kuwa magodauni, wameuza vyuma chakavu, wamepeperusha ajira, wameua mazao ya wakulima kwa kuua viwanda vya nguo, wameua mazao ya mifugo kwa kuua viwanda vya ngozi, viatu, hawajaheshimu mikataba, hawajalipa serikalini, wametajirika kwa kuchukua mali ya umma. Nawambia wakaangalie upya mikataba inasemaje, vinginevyo wajiandae kisaikolojia. 
Link ya Video Inaguata Sooon
Watu wa Igunga wakiri Mwigulu Nchemba ni SOKOINE wa II. Yeye amesema tutaipeleka Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati 2015-2025.
Naibu waziri wa fedha aliyetokea kugusa mioyo ya watanzania masikini na kufufua matumaini yao ndg Mwigulu Nchemba juzi alikonga nyoyo za wananchi wa Tabora waliofurika Igunga kumsikiliza. Mwigulu aliyekuwa akishangiliwa kila alipofafanua hoja aliwaacha wanaigunga wakibaki makundi makundi mpaka giza lilipoingia wangali viwanja vya Sokoine kutafakari hotuba yake iliyokuwa na sura ya kiongozi wa taifa.
Katika hotuba yake Mwigulu alirudiarudia neno "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI IFIKAPO 2025" na kushangiliwa kwa kishindo.
Mwigulu alibainisha kuwa mambo ya msingi kufikia hatua hiyo kuwa ni
1) Maadili na uzalendo wa wasimamizi wa rasilimali za taifa. Mwigulu alisema wanahakikisha kwamba kila fedha inakwenda kutoa huduma iliyokusudiwa, tunahakikisha kodi za wananchi zinakwenda zilipokusudiwa. Tukikusanya fedha kwa ajili ya umeme, tunasimamia iende kwenye umeme, tukikusanya fedha ya barabara tunahakikisha zinakwenda kwenye barabara, hivyohivyo kwenye Afya, elimu nk. Mwaka jana tumegundua tulitoa zaidi ya 48bil kwa ajili ya dawa mawilayan lakkni ni 7bil zilitumika kununua dawa huku kila mgonjwa akienda hospital anahundulika na homa na kuambiwa kanunue dawa kiosk kile, huu ni wizi, kiosk kinatoa wapi dawa ambazo serikali haiwezi kupata kama sio kufanyia biashara dawa zilizonunuliwa kwa kodi za watanzania. Naagiza hili likome na hatua zitachukuliwa, madiwan na vyombo vya dola simamien hili. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"
2) Kuachana na kufanya kazi kwa mazoea. Mabadiliko ni vitendo na yanaonekana kwa kubadili style ya kufanya kazi ili kulinda fedha za umma. Timebadili ulipaji wa mishahara kipambana na mishahara hewa. Tumebaini zaidi ya wafanyakazi elfu kumi na nne (14,000) walioyeyuka tjlipoomba akaunt zao na 1,900 wa keshi nao wameondolewa kwenye malipo. Tumeokoa zaidi ya bilion 40. Naagiza maofisa wote wahakiki watimishi waliopo kazini na walete akaunt. Tukibaini makosa yule aliezembea atafute kazi ya kufanya na hatua zitachukuliwa. Mpaka sasa waliozembea tumewapeleka polisi na TAKUKURU wafikishwe mahakamani.
Tumekagua madai tukagundua udanganyifu, kwenye bilion 500 tumegundua halali ni bilion m100 tu, tumeokoa bilion 400 na tumewapeleka polisi wote waliodanganya. Naagiza wakaguzi watimize wajibu wao kabla ya kuleta madai wizani kwangu. Wakileta tutskagua, Tukigundua udanganyifu aliyeleta hiyo atafute kazi nyingine ya kufanya na tutamburuza mahakamani. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"
3) Tutapunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho kwa kutekeleza vyema sera za kodi. Tutawatoza kodi matajiri ili fedha hizo tuwasomeshe watoto wa masikini. Tutatoza kodi matajiri ili fedha hizo tupeleke huduma za maji, madawa, umeme na barabara vijijini. Hatuwezi kuwasamehe kodi matajiri mabilioni ya shilingi, wakwepe mabilioni ya shilingi halafu sisi tukimbizane na wajane wanauza matembere kulipa ada elfu 20 mashuleni. Tumefuta misamaha kwa matajiri tuache kuwssumbua wajane na masikini kutafuta elfu 20 za sekondari. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"
4) Tutasimamia mgawanyo wa rasilimali ili keki ya Taifa iwanufaishe watanzania wote kwa usawa. Tumebana matumizi ya serikali yasio ya lazima ili fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo. Tutahakiki bajeti za kila taasisi ya umma na kufuta matumizi ya anasa. Hatuwezi kuwa na shirika la umma linatumia fedha kwa anasa huku watoto wakikaa chini. Kupewa kuvuna rasilimali za umma ni dhamana tu sio shamba binafsi na mashirika na taasisi zote za umma mnaokusanya fedha tokea rasilimali za Taifa mlielewe hili. Hatuwezi kuwa na watanzania hapa wanaishi tanzania na wengine wakiishi kama ulaya wakiwa hapahapa kisa wamepewa dhamana ya kusimamia shirika la umma. "TUTAIPELEKA TANZANIA KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI"
5) Tutatoza kodi kwa matajiri, tuwapinguzie kodi walimu na wafanyakazi wengine, tutatoza kodi tuziwezeshe sekta zinazotoa maisha kwa watanzania wengi ili KUONDOA UHUSIANO WA KUKUA KWA UCHUMI HUKU UMASIKINI NAO UKIKUA. Tukiweka fedha kwenye sekta zinazolisha na kuendesha maisha ya watu wengi tutakuza uchumi huku umasikini wa watu wa chini ukipungua.
6) Kuna watu walinunua viwanda vyetu, wamelipa, wamewekeza, wameendeleza, wametengeneza ajira, wameheshimu mikataba, wanalipa kodi nawapongeza sana. Lakini nimeangalia kumbukumbu kwenye mafaili kuna watu walinunua viwanda, hawajawekeza, hawajaviendeleza, wamegeuza viwanda kuwa magodauni, wameuza vyuma chakavu, wamepeperusha ajira, wameua mazao ya wakulima kwa kuua viwanda vya nguo, wameua mazao ya mifugo kwa kuua viwanda vya ngozi, viatu, hawajaheshimu mikataba, hawajalipa serikalini, wametajirika kwa kuchukua mali ya umma. Nawambia wakaangalie upya mikataba inasemaje, vinginevyo wajiandae kisaikolojia.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...