25 September, 2014

MKE WA DK SLAA AJIPANGA RASMI KWA MAPAMBANO, AJIANNDAA KUGOMBEA UBUNGE 2015

Kwa   taarifa  kutoka   watu  wa  karibu   wa   Bi  Josephine    Mushumbuzi  ambaye   pia    ndiye  mke   wa   Dk   Slaa    Katibu    mkuu  wa  chadema  zinasema     mwanamama   huyo   machachari     amejipanga  vya  kutosha   kuingia   kwenye   siasa  rasmi  ambapo  anategemea  kugombea  ubunge  mwaka   2015, Mtoa   habari   amesema   tayari   Bi  Josephine  Mushumbuzi    amejipanga   vya kutosha  kuhakikisaha  anagombea   ubunge  mwaka   2015   Kwasababu    anaamini  uwezo  wa   kufanya  hiyo   anao,  Lakini  mpaka  sasa  haijulikani     atagombea ubunge   kupita jimbo   lipi!
    Habari    zinasema   mipango  ya  mwanamama    huyo    ilikuwa  agombee  ubunge   mwaka   2010 katika  uchaguzi   uliopita   lakini  kutokana  na  ushauri   uliyokuwa  amepewa  na  mume  wake DK   Slaa  ndiyo   maana  alishindwa   kugombea   kipindi  kilichopita  lakini  kwa  sasa  amejipanga  vizuri   kuhakikisha   anaingia  kwenye  mapambano  rasmi   ya kisiasa   kwasababu   siasa   anaipenda   sana  ndiyo  maana   amekuwa   tayari   kupambana na  watu  wanaokichafua chama  hasa  kupitia  mitandao   ya  kijamiii  na  wakati  mwingine   alishawahi   kushiriki   katika   maandamo  ya   chadema   mkoani   Arusha.,
    Taarifa  zaidi   zinasema   kuwa  tayari   mwanamama   huyo   ameisha  unda   timu  maalum   itakayomsaidia  katika  kipindi  cha   uchaguzi, na  timu  hiyo  inaundwa   na   vijana   wengi  kutoka  baraza  la  vijana  Bavicha  ili   kuhakikisha  anashinnda  kiti   cha  ubunge   hasa  pale   atakapoamua  kutangaza  jimbo   atakalo  gombea   2015.
  Jojo The Fighter inamtakia  Josephine a.k.a wajina wangu kila  kheri  katika harakati hizo!!
  

Bi; Josephine   Mushumbuzi    siku   aliposhiriki   maandamano  ya  chadema  huko   Arusha na kujeruhiwa vibaya.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...