Kuna mchezo wa Television (TV game show) unaoitwa “Family Feud,” ambao unashindanisha familia mbili. Familia inayopata points nyingi zaidi, kutokana na majibu yao, inashinda na kupata zawadi.
Sasa huyu mama, mume wake akiwa pembeni kama mshiriki mwenzie, aliulizwa. “Kama ungekuwa na uwezo wa kubadilisha sehemu moja tu, ya mwili wa mumeo, ungebadilisha sehemu ipi?” Mwanamke huyo akajibu “his penis” au “uume wake!”
Kwa kuwa ni kawaida kwa wanawake wa USA kusema wanapenda mwanaume awe na uume mkubwa, na hulalamika kwa rafiki zao wakikutana na mwanaume mwenye “kiduchu,” kauli ya mama huyu ilichukuliwa kumaanisha kuwa mumewe ana “kiduchu;” kitu kilichomuacha host Steve Harvey na wahudhuriaji wamepigwa na butwaa. Walishangazwa na jibu hilo huku wakionekana kujiuliza, mke huyo anaweza vipi kumdhalilisha mumewe mbele ya taifa zima; huku mumewe akionyesha kushikwa na aibu huku akijikaza kisugusugu.
Mwendeshaji(host) wa kipindi hicho mchekeshaji maarufu Steve Harvey akionekana kupigwa na butwaa na kutoamini alichokisikia
Lakini wabishi wamekataa utetezi huo. Wanasema kwamba kwa mwanamke huyo kufikiria hivyo kwa haraka haraka, sababu hakujua kama ataulizwa swali hilo kabla, inaonyesha ana tatizo na nyeti za mumewe. Na kwamba wanawake wengine 100 walioulizwa kwa siri hawakutoa jibu hilo ni ushaidi zaidi kwamba jibu la mama huyo halihusiani na kupata points nyingi, bali alitoa lake la moyoni. Baadhi ya wanaume wanasema wangempa talaka mara moja. Video ya kituko hicho tizama hapo juu.
No comments:
Post a Comment