Thomas Eric Duncan mwanaume aliesafiri kutoka Liberia mpaka Marekani akiwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola amefariki muda mfupi uliopita nchini Marekani baada ya kuwa kwenye hali mbaya.
Pamoja na hayo pia mamlaka husika zinaendelea na jitihada za kuhakikisha ugonjwa huo hausambai nchini humo na wanafahamu kabisa kwamba virusi vya Ebola vinaweza kuishi kwenye miili ya watu waliofariki ndio maana wakati wa kuizika ni watu pekee wenye mafunzo maalum tena wakiwa wamejikinga ndio wanaruhusiwa
No comments:
Post a Comment