Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za serikali (PAC) Zitto Kabwe amemlipua mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Suleimani Nchambi {CCM} kuwa ni kati ya waliohusika kugawa rushwa ya sh milioni kumi kwa baadhi ya wabunge waliosimama kutetea kashfa ya uchotaji fedha sh Bilioni 360 katika Akaunti ya Escrow.

Kulipuliwa kwa Nchambi nje ya Bunge ,kumekuja siku chache baada ya mbunge huyo kuzomewa Bungeni na wabunge wenzake wakati akipingana na ripoti ya kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam jana, Zitto alidai kuwa Nchambi anahusika kuwahonga wabunge kati ya sh milion 3 hadi 10. Alisema Nchambi alikuwa akigawa rushwa hiyo kwa awamu kwani kabla ya mbunge kuingia na kuchangia hoja ya kuwatetea.