Umoja
wa wamiliki magari ya mizigo TATOA umewapa pole wamiliki wa magari,
madereva na wafanya biashara wanaosafirisha mizigo kuelekea Kongo DRC
kufuatia ajali ya moto iliyotokea takribani wiki mbili zilizopita katika
Yadi ya Whiski iliyoko jirani na mpaka wa Kasumbalesa katika nchi ya
Demokrasia ya watu wa Kongo na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.
‘TATOA
inatoa pole kwa familia na waathirika wote wa janga hili la moto kutoka
nchi za Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Congo na Afrika Kusini, na pia
kipekee TATOA inapenda kutoa shukrani kwa serikali ya Congo kwa juhudi
zao za kuhakikisha hali ya amani boda na kazi kuendelea pamoja na
taratibu mpya za kiusalama walizochukua’ alisema msemaji wa TATOA, Bwana
Elias Lukumay.
Akielezea
chanzo cha moto huo, bwana Lukumay alisema taarifa za awali zinaonyesha
mlipuko huo ulitokea baada ya gari la mafuta kukwaruza gari jingine
hivyo kupata nyufa katika Tanki lake la mafuta hali iliyosabababisha
mafuta kuvuja na kutapakaa katika eneo la Yadi na baadaye kushika moto.
‘Tatizo
la msingi ni kuwa yadi ya Whiski haikuwa na vifaa vya kupambana na
moto, na hivyo tunaziomba serikali zetu zinazosimamia vituo vya mipakani
kujifunza kutokea kwenye tatizo hili na hivyo kuchukua hatua stahiki
kuboresha huduma kwenye yadi hizo’ alisisitiza Lukumay.
Bwana
Lukumay pia alisema TATOA imetuma timu ya wataalam kwenda Lubumbashi
kuangalia upana wa maafa, huku pia IKITOA wito kwa makampuni mwanachama
wa TATOA kutoa taarifa kuhusiana na maafa waliyoyapata.
‘TATOA,
ingependa kuona inapata ushirikiano wa karibu kutoka upande wa
serikali, ili kwa pamoja tujipange na tuweze kufanya maandalizi ili
janga kama hili lisije tokea kwenye boda zetu zote siku zijazo’ alisema
Lukumay.
TATOA
pia imeiomba mamlaka ya barabara Tanzania (TANROADS) kupunguza usumbufu
usio wa lazima kwa malori katika maeneo ya mizani hasa katika kipindi
hiki cha mwisho wa mwaka ambapo bandari yetu imejaa mizigo mingi ya nchi
jirani.
No comments:
Post a Comment