04 December, 2014

JELA KWA KUSAMBAZA PICHA ZA MPENZI WAKE!


Sheria ya Carlifonia imepiga marufuku kusambaza picha za mpenzi au mtu yeyeote kama kulipiza kisasi

Mwanamume mmoja mjini Los Angeles nchini Marekani, amefungwa jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza picha za utupu wa mchumba wake kama hatua ya kulipiza kisasi.
Yeye ni mtu wa kwanza kuhukumiwa chini ya sheria inayojulikana kama 'Revenge porn' yaani wanaopatikana na hatia ya kulipiza kisasi kwa kusambaza picha za wapenzi wao wa zamani wakiwa uchi.
Noe Iniguez, mwenye umri wa miaka 36, alipatikana na hatia ya makosa matatu ya uhalifu ikiwemo kusambaza picha za mpenzi wake kinyume na sheria pamoja na kuiuka agizo la mahakama la kumzuia kumkaribia mpenzi wake wa zamani.
Iniguez alitumia jina bandia kutuma ujumbe wa kumchafulia jina mpenzi wake kwenye ukurasa wa Facebook wa mwajiri wake, mwezi Disemba 2013. Yote haya kwa sababu tu mwanamke huyo aliachana naye.
Mnamo mwezi Machi, alisambaza picha ya mpenzi wake akiwa nusu uchi huku akimtusi na kusema ni mlevi na pia kumtaka mwajiri wake kumfuta kazi.
Chini ya sheria ya jimbo la Carlifonia iliyopitishwa mwaka 2013, ni kinyume na sheria kusambaza picha za mtu yeyote akiwa uchi kwenye mitandao ya kijamii na kumsababishia shinikizo la mawazo mtu yule.
Jaji David Fields alimhukumu, Iniguez mwaka mmoja jela pamoja na kumtaka apokee ushauri nasaha kuhusu namna ya kuwatunza wanawake.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...