Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.
Ndege
hiyo ilianguka siku ya alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa
ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame
kusini mwa Somali.Kulingana na msemaji wa Jeshi kanali david Obonyo: Ndege ya KDF iliokuwa ikirudi nchini Kenya baada ya kufanya mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somali,ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kuanguka katika eneo la Kismayu .
Kanali Obonyo hatahivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.
No comments:
Post a Comment