19 January, 2015

MWIGULU ANUSURIKA, APOTEA ANGANI MASAA SITA!

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amenusurika kifo, baada ya kupotea angani kwa saa sita akiwa ndani ya helikopta iliyokuwa inazunguka sehemu mbalimbali mkoani Tanga. Ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano na waongoza ndege, inayotumika katika mikutano yake kwa vile pamoja na uwaziri ni Naibu Katibu Mkuu CCM Bara. Tukio hilo lilitokea jana wakati anatoka Kilindi kwenda wilayani Muheza, kwa ajili ya mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike kwenye uwanja wa Orofea. Kiongozi huyo kabla ya kupata mkasa huo, alihutubia mkutano wa hadhara na alipomaliza alianza safari kuelekea wilaya za Pangani, Mkinga na Muheza kwa ajili ya mikutano. Nchemba alisema kuwa wakati anatoka Kilindi alipoteza mawasiliano na kulazimika kuzunguka angani zaidi ya saa sita. Baadaye rubani alipofika wilayani Muheza, alipata mawasiliano japo walikuwa wamechelewa. Nchemba akiwa ndani ya ndege hiyo alitua salama katika uwanja wa mpira wa Jitegemee wilayani Muheza ambapo alipokelewa na mwenyeji wake mbunge wa jimbo la Muheza Herbert Mntangi (CCM) na Mkuu wa Wilaya ya Subira Mgalu. Akiwa katika mkutano, alisema kuwa watahakikisha tatizo la maji katika mji wa Muheza linamalizika na kwamba katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 watatenga fedha za ndani bila kujali wahisani.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...