21 January, 2015

TSH. MILIONI 3 KUTOLEWA KWA ATAKAYEMPATA MTOTO ALBINO ALIYETEKWA!

Polisi wa Tanzania wamesema watatoa tuzo kwa yeyote atakayetoa taarifa utakaoweza kusaidia mtoto wa kike albino ambaye hajulikani alipo anayehofiwa kutekwa kwa lengo la kupata viungo vyake vya mwili. Pendo Emmanuelle Nundi, mwenye umri wa miaka 4, alitekwa mwezi uliopita. Baba wa binti huyo ni miongoni mwa watu 15 waliokamatwa kutokana na kutekwa huko. Viungo vya mwili wa albino, husakwa na waganga wa kienyeji. Tanzania imewapiga marufuku waganga wa kienyeji wanaopiga ramli katika jitihada za kuzuia mashambulio dhidi ya albino. Polisi wameahidi kutoa shilingi milioni tatu za Kitanzania sawa na $1,700 kujaribu kumtafuta binti huyo ambaye hajulikani alipo “mfu au hai”. Wajomba zake wawili binti huyo nao pia wamekamatwa kama sehemu ya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...