28 April, 2015

ZAIDI YA 4000 WATHIBITISHWA KUFA NEPAL

Utawala nchini Nepal unasema kuwa watu zaidi ya watu 4000 wamedhibitishwa kuaga dunia huku wengine 8000 wakijeruhiwa kwenye janga la tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa siku ya Jumamosi.
Jitihada za uokoaji zinaendelea kukiwa na matumaini ya kuwapata manusura, lakini jitihada hizo bado hazijayafikia maeneo mengine yaliyo mbali.
Watu wengi walilala nje kwa usiku wa tatu mfululizo kwenye mji mkuu Kathmandu wakihofia kutokea kwa mitetemeo mingine midogo.
Serikali ya Nepal inasema kuwa inahitaji kila msaada ukiwemo wa mablanketi , helkopta, madaktari na madereva. Kuna uhaba wa maji, chakula na umeme huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...