16 May, 2015

MAMBO 10 HATARI CCM KUNG'OKA MADARAKANI

Wakati chama cha Mapinduzi (CCM) kikitarajiwa kuanza vikao vyake kuelekea uchaguzi mkuu mwanzoni mwa wiki ijayo mjini Dodoma, mambo muhimu 10 yametajwa kuwa ndio hatari zaidi yanayoweza kuking'oa chama hicho katika utawala wa nchi kwa mara ya kwanza katika historia. 

I. UFISADI
Wimbo huu wa ufisadi ambao ulianza kuandama serikali ya CCM tokea ilipoingia madarakani 2005 kwa kuhusisha kashfa mbalimbali za upotevu wa mabilioni ya fedha katika sekta mbalimbali za umma zimekuwa zikitumiwa na wapinzani kama fimbo ya kuichapa kuonyesha udhaifu wake. 

2. KUTOWAJIBIKA
Chama tawala pia kimekua kikilaumiwa kwa kutosimamia vyema uwajibikaji wa serikali inayoiongoza kwa mambo mengi kwenda ndivyo sivyo lakini bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wazembe.

3. WAGOMBEA WASIOTAKIWA NA WANANCHI.
Mara kadhaa katika chaguzi mbalimbali hasa mwaka 2010 CCM imekua na tabia ya kuwaacha wagombea ambao ni chaguo la wananchi na badala yake kuwaweka wanaotakiwa na vigogo wa vikao vya juu.

4. MAKUNDI
Hakuna siri kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa na desturi ya kuwepo kwa makundi miongoni mwa wanachama wake kuelekea uchaguzi mkuu kwani kila mmoja huwa na wafuasi wake wanaomuunga mkono.

5. KUPAKANA MATOPE
 Tofauti na desturi ambapo chama tawala humaliza tofauti za makada wake ndani ya vikao, msimu huu umeonekana wa wanachama na hasa viongozi kupakana matope waziwazi kuelekea uchaguzi wa Octoba.

6. CHAMA KUDAIWA KUMEZWA NA MATAJIRI
Duru za kisiasa zinadai kuwa chama hicho kinaonekana kuacha muelekeo wake wa kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi ambapo sasa kinaonekana kushikwa na matajiri huku baadhi ya makada wake wakilalamika kuwa fedha imekuwa kigezo cha ushindi ndani ya chama.

7. SIASA ZA UHASAMA
Kaka ilivyosemwa katika kipengele cha 4 juu ya kuwepo kwa makundi ndani ya CCM kuwa siyo jambo la siri, uchaguzi unaonesha makundi ya kipindi hiki yamegeuka kutoka kwenye siasa na kuwa ya u hasama ambao ni kitisho kikubwa pale linapokuja swala la kuvunja makundi na kujenga umoja ili kupata ushindi.

8. UKOSEFU WA AJIRA
Moja ya kauli za kutia matumaini alizoingia nazo Raisi Kikwete madarakani ni pamoja na ahadi ya ajira kwa vijana waliopoteza matumaini, ingawa maofisa za JK wamesema zimepatikana ajira milioni 2 mara mbili zaidi ya alivyoahidi lakini ukweli ni kuwa Taifa liko katika wakati mgumu kutokana na vijana wengi kushindwa kupata ajira rasmi.

9.MAANDALIZI DUNI YA UCHAGUZI.
Mazingira yanaonyesha kutowepo kwa maandalizi stahiki ya uchaguzi tokea tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) mfano fedha za kugharamia uchaguzi, uandikishaji unao sua sua wa kupiga kura, elimu ya uchaguzi na ukosefu wa vitendea kazi vya uchaguzi, vyote hivi vinaweza kuiweka pabaya CCM.

10. KUTOTEKELEZA AHADI KWA ASILIMIA 100
Jambo la mwisho linalowezakuwa hatari kwa CCM ni kutotekelezwa kwa asilimia 100 kwa ahadi zilizotolewa kwa uchaguzi uliopita, mfano wa ahadi hizo ni maisha bora, mahakama ya kadhi na uboreshaji wa huduma za jamii.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...