Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’. Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemwalo lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba kumeonesha vithibitisho vya picha na kujiuliza ni kwanini wasanii hawa wamekumbwa na hili...
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
TANZANIA:
1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy!
2.Ali Kiba
Iliwahi kusemekana pia kuwa Ali Kiba ni Freemason, na wewe pia unaweza kufikiria sababu kwamba eti alikuwa maarufu sana na baadae kufifia. Maoni ya mwandishi (Hakuna uthibithibisho/ushaidi unaoweza kuwekwa thidi yake).
3.Jacquelin Wolper
Ni muigizaji maarufu wa kike Tanzania. Maoni ya mwandishi ( Hakuna ushaidi, tetesi peke yake hazina umuhimu)
KENYA:
1.Camp Mulla
Maoni ya mwandishi (Hapana, sio kweli. Sababu ya kufanikiwa kwenye muziki haimaanishi kuwa ni members wa Freemason. Hakuna mtu mwenye ushahidi kuwa Camp Mulla ni members wa Freemason).
2.Octopizzo
Maelezo yanayomhusu yanaonekana kuwa mengi sana kama kawaida, ni moja kati ya wasanii ambao tetesi za kuwa illuminate ni nyingi zaidi.
3.Nonini
Ukimtaja Nonini kama Illuminati lazima kitu serious zaidi kiandikwe ama ikielezwe. Nonini sio Illuminati (maoni ya mwandishi).
Hao ndio waliandikwa na kutolewa maoni ama maelezo na muandishi wa mtandao huo. Lakini tetesi huwa nyingi na kuongezeka mara kwa mara kwani hata Avril pia huwa anatajwa kuwa Illuminati na kwamba kazi yake ni kueneza usagaji nchini humo na eti sababu mojawapo ni mashairi ya wimbo wake ‘Chokoza’.
Haya yote yanasemwa tu, cha kufanya ni kile alichokisema Prof. Jay kwenye wimbo wake ‘Bongo Dar es Salaam’…
Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600
wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na
watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni
mwao wapo viongozi wa serikali.
Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande.
Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo. Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.
Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya 600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.
Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.
Chande alizungumza na mwandishi wa habari katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.
Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.
Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa amejiunga na kundi hilo!!!

No comments:
Post a Comment