26 June, 2015

ISSUE YA FAIZA ALLY KUNYANG'ANYWA MTOTO NA MBUNGE SUGU, ALITUMIA SIKU MOJA MAHAKANI KUSHINDA KESI!



                                                            MR II SUGU NA MTOTO WAKE

Imeendelea kuwa ishu ambayo kila mtu anaiongelea kwenye kona yake anachokiona sahihi, wapo wanaokosoa Mahakama kuamisha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupatiwa mtoto wake na Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenzake.

Wa kwanza kuwasha kipaza sauti alikuwa Mbunge Martha Mlata >>> “Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”>>>

Ukaja muda wa Mbunge David Kafulila >>> “Hii nchi ina mihimili mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali… Tuheshimu maamuzi ya Mahakama”>>>

Waziri Saada Mkuya alikuwa wa mwisho kuongelea ishu hiyo hiyo >>> “Kama mama na mimi nilipoisikia ile taarifa nilipata uchungu, kila binadamu ana mapungufu yake lakini mtotto alelewe na mama yake”>>>

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...