Staa
wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na
William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’
kiukoo.
MREMBO anayefanya
poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’
kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye
William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’
kiukoo.Ndani
ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi
wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake
jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini
hapo.
Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba.Mbali
na kunaswa siku hiyo, pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara
kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe
jijini Dar.
Mara
ya mwisho, Linah na Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji
wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar, mapema mwezi huu.
Ndani ya Triple 7, paparazi wetu aliamua kumfuata Linah ili ajiridhishe
uwepo wake na mwanaume huyo ambapo msanii huyo alijing’atang’ata na
kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa natoka naye. Sijui umenielewa? Natoka naye
sehemu mbalimbali.Ila kukutoa wasiwasi tambua kwa sasa sina mpenzi na
nina haki ya kuwa naye, sina mpaka wa kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.
No comments:
Post a Comment