26 June, 2015

WOLPER: MIMI NI FREEMASON KWA MUDA MREFU SASA


92d27__wolper2bongoclan.co_.tz_Staa wa bongo movie Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’.

UPO? Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake.
Jackline-Wolper2Jacqueline Wolper Massawe akiwa katika pozi.
Wolper alisema ni kweli yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama wengine.
“Freemason si ni taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi kuwa mwanachama? Tena nataka nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini halisi wa Freemason kwa muda mrefu sasa,” alisema Wolper.

GPL

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...