14 July, 2015

PICHA HII INATUFUNDISHA NINI KUHUSU WATAWALA WANAO OMBA KUPEWA MAMLAKA KWA MUHULA WA PILI.

Monduli Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada kumalizika kwa likizo Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo wilaya ya Monduli mkoani Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa jengo la shule ya Msingi Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na kusababisha maafa kwa wanafunzi.

Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64 kutoka Monduli mjini iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji waliojitoa haina milango na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya vumbi na baridi kali hasa kipindi cha mvua. Wanakijiji hao wamesema kuwa hali mbaya ya miundombinu ya shule hiyo imewafanya wazazi wengi kusita kuwapeleka watoto mashuleni hivyo ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze kusaidia kutatua changamoto hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu Kutetei amesema kuwa licha ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji jambo linalokwamisha maendeleo ya taaluma shuni hapo.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wafugaji la Monduli Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto Sanare ameeleza kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule hiyo hivyo kushiriki katika ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba serikali isaidia shule hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.

Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika masuala ya elimu tofauti na miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu ikiwemo kukosekana kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba wa maji na vifaa vya kufundishia na nyumba za walimu

My take
Swali: Kweli Kabisa tunaamini watu hawa wanaweza saaaana kuongoza? Kabisa wapo wanaosema tuwape miaka mingine mitano tena kwa macho makavu kabisa....

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...