Ile Safari ya matumaini ya Mh Edward Lowasa sasa imefika ukingoni baada ya fununu [rumours] kwenye mitaa na vyumba vya habari na wanahabari Dar es Salaam na Dodoma kusheheni mijadala na minong'ono na hata maelezo yenye sifa zote kuwa sasa ile safari ya gwiji wa siasa za kwenye vyombo vya habari [media] imefika TAMATI.
Ni safari iliyokuwa na mvuto wa aina yake iliyosheheni mambo mengi yenye kuamsha maswali magumu yenye kuitaji majibu mazito. Ni safari ya matumaini ya Mh Edward Ngoyai Lowasa iliyoibua mazungumzo mengi yaliopelekea SIASA za NCHI kuzungumza habari za WATU na si habari za maswala [Issues].
Binafsi sikuwa mpenzi au shabiki wa safari ya matumaini kwa kuwa sikufanana nayo KIITIKADI NA FALSAFA YAKE.Ilikuwa safari iliyosheheni majina makubwa sana kwenye siasa za Tanzania mfano wa majina makubwa kama viongozi wakuu wa kichama wa Mikoa na Wilaya, Wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya Mawaziri walio hudumu kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye awamu zote lakini wengi wao wakiwa ni wale ambao utumishi wao ulionekana kuwa na sintofahamu nyingi zilizoibua kukosa tunu ya utumishi ulio tukuka, yani utumishi wa bila mawaa.Kwa timu hiyo kuwa na watu wenye ukwasi mkubwa na wazoefu wa mambo ya Kitaifa safari hiyo inapoishia hapo pasipo kufika kwenye kilele basi kuna jambo ambalo Watanzania kwa ujumla wetu mara baada ya Wanaccm kumpata mgombea wao tarehe 12/07/2015 basi ni dhahili vyombo vya habari na social media zote zitapata kuchambua na hata kupata UKWELI ya yaliokuwa yanajili ndani ya safari hizo zilizokuwa zimezungukwa na mbwembwe nyingi sana.
Hakika kwa hali inavyoendelea kwenye viunga vya JIJI LA DODOMA safari hii sasa inaangaza kwa watu ambao ukisoma alama za nyakati wao wako katika kuhahakikisha wanapata kuungwa mkono na Wanaccm wapewe nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi ambayo pasipo na shaka wao hawana vikwazo vyovyote na zaidi na sifa ambazo zinawapa maksi kwa hali na mali kuwa kwa jinsi Taifa lilipofika hapa ukilinganisha tuliko tolewa na mwasisi wa Taifa hili Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mpaka hapa tulipofika basi kuna jambo haliko sawa na linaitaji mtu makini sana ambae anasifa zote za kuhahakikisha Tanzania njema inaludi mikononi mwa Watanzania.
Kwangu binafsi na jicho langu ambalo nimeliwekeza zaidi na kwa dhati kabisa kwa mtia nia CHARLES MAKONGORO NYERERE naendelea kuamini kuwa jicho ilo linaangazwa pia na Watanzania walio wengi ambao wana muitaji kiongozi makini kuongoza Tanzania.Tanzania yenye HAKI SAWA na fursa zenye kuinua raia wote kimaendeleo na kupinga kwa dhati Rushwa na Ufisadi na kudumisha Uadilifu na Uzalendo wa Taifa.
Hivyo kufika mwisho kwa safari ya matumaini kunaibua mwanzo wa siasa nyingine mpya na hivyo zile siasa za mitandao [Makundi] kuwa na KIFO kisicho rasmi katika siku hizi chache zilizobaki kufika tarehe 12/07/2015.Hakuna Mtanzania yoyote kwenye Taifa letu asiyejua madhara [IMPACT] ya siasa za mitandao [makundi] ambazo zilinawili sana toka mwaka 1995 na hivyo kulifanya TAIFA kuegemea kwenye siasa za nani ana mfahamu nani na sio kuangalia uwezo wa binafsi [Content] wa mtu katika kutenda mambo yeney faida kwa Taifa.Hatimae JIPU limepata upasuaji .
KUPITIA VYOMBO VYA HABARI VYA MAGAZETI TAARIFA
1: Uhuru
Front Page ''Waliokiuka Kanuni ''out''.-Hiki ni chombo kikubwa sana cha CCM
2:Rai
''Lowasa afitiniwa''
3: Shuhuda
''Kikwete Atajwa ''KUMMALIZA'' Lowasa.
4: Umma Tanzania
''Kiwewe Kambi Ya Lowasa''
Front Page ''Waliokiuka Kanuni ''out''.-Hiki ni chombo kikubwa sana cha CCM
2:Rai
''Lowasa afitiniwa''
3: Shuhuda
''Kikwete Atajwa ''KUMMALIZA'' Lowasa.
4: Umma Tanzania
''Kiwewe Kambi Ya Lowasa''
No comments:
Post a Comment